Radio ya gari kuandikwa kijapani

Radio ya gari kuandikwa kijapani

dagii

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2013
Posts
4,959
Reaction score
3,778
Wakuu hivi majuzi niliagiza gari kutoka Japan sasa kuliwasha na kutembelea si tatizo, tatizo ni hapo kwenye radio imeandikwa ki Japanes na tatizo ni kuiwasha sasa na mwezi sasa siisikilizi, kama kuna mjuzi tafadhali msaada wakuu.
 
nenda kaipaki maeneo ya tandale, after 15 mins utakuwa on ur way to have a new english radio.
 
Kama vipi jiunge na tuition ya lugha ubalozi wa Japan au toa hiyo ununue nyingine.
 
Badilisha uweke nyingine Mkuu, kwanza redio zinazokuja na gari masafa yake yanakuwa madogo.
 
Mkuu dagii nijuavyo kitufe cha kuwashia(power on/off), mara nyingi huwa kikubwa kuliko vingine japo pia kinaweza kuwa kidogo, huwa kinatengwa kidogo tofauti na vingine, hakiwekwagi katikati ila pembezoni mwa kifaa husika(redio). Kwa ujumla si kitufe rahisi kukikosa, jaribu tena au labda ina tatizo katika uwakaji wake au uunganishwaji. Ukishindwa kabisa jaribu kuweka picha watu wanaweza kukusaidia kabla mafundi hawajaenda kukutoa pesa ya kukuelekeza tu.
 
Last edited by a moderator:

Umemuelewa mtoa hoja?.
Mi kama nimemuelewa maelekezo ya kwenye redio yote yameandikwa ki japani na si kwamba anashindwa/hajui pa kuwashia. Tatizo hili lipo pia kwenye radio zote zinazo kuja na toyota harrier toka kiwandani. Zina mpaka road/streets maps zikionyesha maeneo mbalimbali lakini lugha na maelekezo yote ni kijapan.
 
Wakuu hivi majuzi niliagiza gari kutoka Japan sasa kuliwasha na kutembelea si tatizo, tatizo ni hapo kwenye radio imeandikwa ki Japanes na tatizo ni kuiwasha sasa na mwezi sasa siisikilizi, kama kuna mjuzi tafadhali msaada wakuu.

Solution ni mbili
1.jifunze kijapan
2.badilisha weke radio yenye lugha unayoielewa,probably english
 
Ingekuwa ni Tanzania tunatengeneza magari kwa ulimbukeni wetu tungeweka lugha za kiingereza.
 
Sio ulimbukeni mkuu,inategemea mnunuzi mkuu ni nani! Yatakayouzwa ndani yataandikwa kiswahili na yatakayouzwa nje ya iitawekwa lugha maarufu! Hao wajapani wenyewe yenye kijapan ni ya hapohapo Japan ila mengi ni kiingrreza. Hata BMW au Audi nyingi zina kiingereza
 
Suluhisho ni Hili,
Download application ya Google Translator. Washa radio piga picha itakutafsiria unachotaka.

Note: Google translator unaweza tumia keyboard kuingiza maneno upate tafsiri au Camera,unapiga picha unapata tafsiri.
 
Back
Top Bottom