Radhi ya baba na mama ndani ya safari yangu ya Saudia

Wala hakuna sababu ya kulazimisha iishe leo labda uamue tu, we relax fanya taratibu , toa kitu bora wasomaji tutasoma tu hata ichukue miezi

Kusoma ni kipaji, asiye na kipaji atakusumbua sana
Dah! Afadhali broo maana naona like I was being pressurised
 
Huwezi kujua nini kinacho zungumzwa maana wewe si Muislam kaka hujui ukubwa wa ibada hiyo !!!
Una maanisha nini??? Bandiko lipo kwa ajili ya kila mtu mkuu, hata baadhi ya waislam hawajui hata madudu gani nayaongelea hapa
 

Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano


Jaribu kufuatilia mtiririko wa namna huyu bi mkubwa anavyoonesha mahali ilipo lastest update
hiyo stor ni nzuri nikaisome?
naionaga napita tu
 
.......Kama ambavyo kwenye ukristo kuna catholic, protestants, Lutherans etc etc ndivyo hivyo hivyo kwenye uislam kuna madhehebu, makundi makubwa yakiwa ni sunni na shia, hawa shias hivi karibuni wamengia Tanzania na kuanzisha redio zao ikiwemo radio maarufu kule Tanga inayoitwa "Radio Maarifa" ambayo mzee wangu anapenda sana kuiskiliza vipindi vyake. Na amekuwa anawa-support sana hawa jamaa!

Kwa wasiofahamu tu ni kwamba, mgawanyiko wa Sunni na Shia umetokana na msingi mkubwa wa fikra za nani alipaswa kuwa kiongozi baada ya Mtume Muhammad (s.a.w) kufariki. Sunni wanasema Aboubakar (R.A) ndio alipaswa kuwa kiongozi kama ambavyo alikuwa na Shias wanasema Ali (R.A) ndio alipaswa kuwa kiongozi. Hapa ndipo mzizi wa makundi haya ulipotokea. Kwa hiyo hawa shias (baadhi yao) hawawakubali kabisa kiongozi wa kwanza, wa pili na wa tatu wa uislam duniani baada ya mume kufariki. Viongozi hao ni (i) Aboubakar (R.A) (ii) Umar (R.A) na (iii) Othman (R.A) kwa wanahistoria watakumbuka huyu ndio alikuwa chanzo cha kupatikana Ottoman Empire.

Sasa bhana wakati tunatoka na mzee kupitia pale kwenye makaburi ya mtume na Aboubakar na Umar, alimtolea salamu mtume kwa kusema (Asalam alaykum yaa rasula Llah) yaani amani iwe juu yako iwe mtume wa mwenyezi mungu, halafu alipofika kwa Aboubakar na Umar akasema tu (asalam alaykum ya ahlul kubuur) yaani amani iwe juu yenu enyi watu wa makaburini. Huu ni mfumo ambao wanautumia sana Mashia, na wakati mwengine hata kuwasalimia hao wawili pia hawawasalimii. Hivi aliona tabu gani kuwataja kwa majina yao na sifa zao???

Kabla marehemu babu hajafariki niliwahi kwenda kumshtaki baba yangu kwake juu ya misimamo yake kuhusu Shias na aliitwa na baba yake (babu yangu) kuulizwa juu ya tuhuma hizi na akazipinga. Ila katika safari hii ndio nilithibitisha kwamba mzee anao muelekeo kamili juu ya hawa watu. Tulipotoka tu nje ya msikiti mimi sikulaza damu wala sikusubiri duku duku langu lipoe, nkamwambia mbona hujatoa salam kwa Aboubakar na Omar kwa mujibu wa sifa zao?? akaniambia wapi nlipoamrishwa nifanye hivyo?? mjadala ukawa mkubwa na mzito mpaka tulipokutana na mama at our self selected meeting point. Mama akajua enheee mabishano ya sunni na shia yameanza kama kawa. Bi mkubwa alikuwa hapendi sana hiyo hali maana mara zote ilimpelekea mzee kukasirika. Mimi nilikuwa nashindwa kukaa kimya maana kwa maoni yangu nilikuwa naona kabisa mzee hayuko sawa. Siku yetu iliharibika pale na ikabidi nimkwepe mzee for the reminder of the day asije akaja akanitolea maneno mazito bure.

In the evining I went to buy food na vyakula ni bei rahisi kabisa pale Madinah. Huu ni mji ambao kwa mujibu wa uislam mtume aliuombea uwe na amani na wametajwa mara kadhaa ndani ya Qur an watu wa mji huu (ahlu al Madinah). huu ni mji wa kiibada zaidi na sio mji wa kiserikali. Watu wake pia ni wakarimu sana.

Siku ya pili ilibidi tukatembelee eneo lililopiganwa vita ya kwanza kabisa baada ya mtume kuhamia Madinah, vita hii inaitwa vita ya Uhud na iliitwa hivyo kwa sababu ilipiganwa katika eneo lililoitwa Uhud. Ni kama vile vita ya Kagera ilivyoitwa hivyo.
Historia inaonyesha katika vita hii Waislam walikuwa bado hawajajipanga vizuri ndani ya mji wao huu mpya ambao walihamia bada ya kuhama Makkah ambapo watu wasio waislam wa Makkah waliwafurusha katika mji wao. Kwa hiyo baada ya Muhammad (s.a.w) kuhamia Madinah, alihama na watu wengi tu waliomuunga mkono, kitendo hiki kiliwakasirisha watu wa Makkah na ndipo walipoamua kwenda kumtafuta Muhammad huko huko Madinah auliwe ili mzizi wa fitna uishe. Maana yeye ndio aliotuletea hizi habari za Uislam.

UHUD BATTLE FIELD

View attachment 1131641

Habari zilimfikia Mtume kwamba kuna jeshi linakuja na akaamua na yeye kuandaa jeshi na vita vikapiganwa. Katika vita hivi waislam walipewa maagizo ya kukaa kwenye kamlima flani hivi na wasishuke huko mpaka mtume (kama kiongozi wa vita atakapotoa amri ya kushuka)

Vita vilianza na waislam wakawa wanaelekea kushinda, walipigana mpaka wapinzani wao wakaanza kurudi nyuma na kukimbia sasa, jeshi lililosaidia na wale watu waliopangwa juu ya kimlima ambao wapinzani iliwawia vigumu kuwa-attack kwa silaha zao ambazo kipindi hicho ni mikuki na mishale. Baada ya kuona vile waislam waliokuwa kwenye battle field wakaanza kukusanya ngawira na mateka, waliokuwa kwenye mlima wakaona choyo na tamaa ikawapanda kwamba watakosa ngawira hivyo wakashuka ili wawahi ngawira. baada ya kushuka mmoja wa majemedari mahiri kabisa akiitwa Khalid Ibn Waalid aligundua hilo na kuwaambia wenzie hawa jamaa wameshuka. wakafanya utaratibu wakapanda kule juu wakaanza kuwashambulia waislam. Waislam walichezea kipondo heavy sana hapa! walipigwa kweli kweli mpaka mtume alitumbukia kwenye shimo moja lililochimbwa kama handaki before war started na kwa namna alivyoanguka alijichoma na sumari la lile kofia la vita (ambayo yalikuwa ni ya chuma hapo zamani) katika shavu lake na kumuachia jeraha. Muslim war front liners wote waliparaganyika na kukimbia huku na huko. Inasemekana kuna waislam waliojitoa muhanga na kupanda kule kule mlimani kwenda kupambana na wapinzaniu wao maana lile ndio lilikuwa eneo la ushindi wa vita. Walipofanikiwa kuwashusha kule mapambano yaliendelea na hatimae waislam wakashinda ile vita.

Waislam wote waliofariki katika vita hivyo walizikwa kwenye eneo hilo hilo na makaburi yao yapo mpaka leo na ndio hayo hapo chini yaliyozungushiwa uzio wa matofali.

View attachment 1131643

Baada ya vita, kile kikundi chote kilichopangwa juu ya kimlima kile walikuwa wanafeel guilty sana na kupelekea (over time) mpaka baadhi yao wakapatwa na maradhi ya wasi wasi amabyo yalichukua uhai wao.

MLIMA AMBAO ILIKUWA NI STRATEGIC POINT DURING WAR

View attachment 1131644

Kwa kweli nilijifunza mambo mengi sana! Baada ya kurudi hotel siku ile wazee wakanieleza kwamba hawakuwahi kuwaza kwamba ipo siku watafika maeneo hayo. Waliishia kusoma tu kwenye historia ya vitabu vya dini na leo mola wao amewaneemesha neema hiyo kubwa. Mama aliniombea dua kila dakika na nakumbuka nlikuwa nkimuomba mama please ukimaliza swala niombee dua ananiambia "hujui tu mwanangu namna ninavyomshukuru mungu kunifanya mimi kuwa mama yako" katika maisha yangu sijawahi kuwaza kwamba nitafika sehemu hizi ambazo najua mtume wetu amefika pia. Ninaposwali nakuombea mwanangu Alllah akupe umri na nguvu, baada ya safari hii ya Umrah utulete tena Hijjah mungu akipenda. Nikifa leo hii mwanangu basi nipo radhi na wewe na naamini tutakutana tena peponi.

Niliwashkuru wazazi wangu kwa kunilea vyema na kunipatia elimu ya dini ambayo ndio drive na inayonifanya nione kwangu hakuna cha thamani katika dunia yangu zaidi ya mama yangu na baba yangu!

Hii ilikuwa ni siku yetu ya tatu kuwepo pale na tulikuwa tumebakisha siku mbili tu ili tuelekee madinah!

Siku iliyofuata nikaamua kuwapeleka wazee wakale bata kidogo, mzee wangu ni wale wazee wa kizamani! unakwenda nae sehemu mnaagiza msosi lakini kama ni bei kubwa analalaamika sana hata kama pesa hatoi yeye. Nakumbuka kipindi flani nilikwenda nae Handeni tulikuwa na keshi. Tukanywa chai kwa mama ntilie mmoja hivi na chapati zao nadhani mnazijua, ukiinua juu na kutizama through unaweza kuona upande wa pili. Basi baada ya kumaliza chai mama ntilie aliposema chapati ni 500/= mzee aligomba sana, aliangusha tifu la maana mpaka nkaskia noma, anasema chapati zile haziwezi kuwa jero labda 300 tu. Nkamtuliza kwa kumwambia mzee the world has changed, it's no longer your age. Hahahahhahhha

Katika piatapita zetu mzee aliishia kuangalia vitu na kuacha bila kuchkua chochote akilalama kwamba bei ni juu sana, mimi nikamwambia bi mkubwa just take whatever you want.

Faraja ya hali ya juu linijia pale ambapo wazee walikuwa wakicheka na kukumbatiana huku wakitaniana barabarani. Mzee anamtania mama kwamba hawezi kuongea hata na maaskari huku akimuuliza in case ukipotea utaomba vipi msadaa japowa kueleekezwa hotel ilipo??

MY PARENTS HAVING GOOD TIMES IN MADINAH
View attachment 1131664

View attachment 1131666

View attachment 1131668

View attachment 1131672


Baada ya siku zetu tano kuisha, ilitubidi tuondoke Madinah kuelekea Makkah ambako ibada rasmi ilitakiwa ifanyike. Maandalizi ya safari yalikuwa tayari tayari na kufika saa nne asubuhi ALI alikuwa keshafika hotelini kwaajili ya safari ya Makkah.....

Makkah tulitahadharishwa juu ya kuwa ndio mji mtukufu kuliko yote duniani kwa mujibu wa Uislam, tusitegemee kukuta ukarimu kama wa Madinah, watu wa huko ni mission towns na ukilala tu wamekuramba hahahahahhahahahah.

Nini kilitokea on our first day in Makkah?????

ITAEDELEA..........................
Nimeangalia picha za wazazi hapo umenifikirisha sana. I wish! one day
 
Back
Top Bottom