Quotes from Dictator Iddi Amin Dada

Lengo la ujumbe ni kuwa kila mtu achunge anachoongea ,ukiongea ukishamaliza kuna KIMOJA kati ya mawili chaweza kukupata
1.Kupigiwa makofi au
2.kupigwa makofi

Kipi kitatokea UKISHASEMA IDD AMIN ndicho alisema I CANT GUARANTEE
He couldn't guarantee because he was a dictator, what did you expect him to say?
 
Wewe lazima ukamatwe sasa,unamfananisha Mh. na hilo nduli, ngoja niwatonye vijana wa kazi, huna adabu kabisa, ulitegemea utapata udc wa Ubungo umetoswa sasa unaanza kashfa.
 
Alikuwa mojawapo wa wanadamu wenye miili mikubwa lakini akili ndogo kama ubongo wa samaki. alikuwa mfano wa bogus kabisa kabisaaaa. ukimsikiliza anaonyesha picha halisi ya mtu aliyekosa elimu na hajui kama hajui.

Alikuwa na akili sana ila matumizi ndio alitumia akili vibaya,
Akili Ni jinsi utapenda zitumia wewe
Power is nothing but control.
 
Tatizo wote mmekubari fitina na chuki za wazungu juu ya Alhaj IDDY AMIN akuwa km hvyo wanavyomueleza maana wazungu aswa wa Israel kuona wamekosana nae ndio wakaona wamshafue km ilivyokuwa kwa Baba baada swaiba wake kutolewa madarakani ndio akaona tuanzishe ile vita ambayo ndio sababu kubwa pia ya umaskini wetu leo
 
Kinachosikitisha ni kwamba Watanzania tulikuwa mstari wa mbele kusaidia wenzetu katika ukombozi barani Afrika kiasi kwamba hata Waganda tuliwaondolea kadhia ya dikteta Idi Amin lakini leo tunamlea wa kwetu. Tunashangilia ndugu zetu wakipigwa, kulemazwa na hata kuuawa na vyombo vyetu vya usalama tunaowalipa kutulinda.

Ndugu zetu wanakamatwa na kuteswa na wale wawakilishi tuliowachagua wenyewe tunafurahi wakinyanyaswa na viongozi uchwara wa kuteuliwa. Hivi leo Idi Amin angekuwa hai tungekuwa tunamwimbia nyimbo za kumsifia na bila shaka tungeshampokea kwa vifijo akifanya ziara hapa kwetu kama tunavyowapokea madikteta waliotuzunguka.

Whither to? Tunaelekea wapi ndugu zangu? Tulimpinga mkoloni ndani na nje ya mipaka yetu, tuliwalaani wakoloni weusi kama Bokasa na Nguema...lakini leo tunawapigia makofi Museveni, Shein na Nkuruzinza. Tunashangilia ndugu zetu na majirani wakiwashughulikia wanaotofautiana nao kimawazo na sasa yanaanza kutupata.

Katiba inasiginwa kwa kisingizio cha eti kunyosha nchi na tunapiga vigelegele. Watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha huku tukiimba hapa kazi tu. Wakati wa Idi Amin ilifikia hadi mamba ziwani victoria walikula nyama za watu hadi kukinai na maiti zilizowazunguka zikielea wakawa wanazitazama tu...so sad!

[HASHTAG]#freemaxcencemello[/HASHTAG] now!
Nilipomaliza kusoms hii
post ilibidi niangalie aliyeiandika..lahaula, ameandika mtu ninayemheshimu mno kwenye hili jamvi.
Nchi yetu ni imara sana pamoja na mapungufu ya hapa na pale kiuongozi lakini hatujafikia sehemu ambapo Shein anafaninishwa na Nkurunzinza. Hapana kubwa mkuu wangu Mag3
 
Back
Top Bottom