Habari wanajf, leo nilibahatika kuangali EATV kipindi kinaitwa 5 selekt (siyo select). Msanii Queen darleen alikuwa studio anahojiwa, aliulizwa ni msanii gani alimvutia kuingia kwenye muziki (inspirational artist or role model). Akajibu kuwa nje ya nchi ni EVE lakini hapa bongo alisema hakuna kwakuwa yeye alipoanza hakukuwa wasanii wa kike zaidi yake na Jide!! Nilijiuliza hivi yeye na unique dadaz, zay b, sister p na wengineo nani alitangulia?! Hata rah p nafikiri ni mkongwe kwake. Namshauri awe anajiandaa na studio interviews, asikurupuke. Asanteni.