QUALIFICATION AND EXPERIENCE

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Joined
Nov 6, 2015
Posts
46
Reaction score
18
naomba kujuzwa,
kwenye ajira za utumishi unaweza kutumia academic trancsript tuu bila ya kua na certificate(bachelor dree) ?
na maanisha kwa wale vijana waliomaliza masomo mwaka huu(2018) matokeo tayari ila certificate bado.
 
Haaa kuna organisation nyingi za kimataifa yaan requirement wanatakaga CV na Cover later basi sasa si unaweza kuwadanganya
 
Utaanzaje kuweka Transcript bila cheti usipoteze muda subiri cheti ....#Unaweka cheti afu pia na transcript kama huna cheti subiri cheti
 
naomba kujuzwa,
kwenye ajira za utumishi unaweza kutumia academic trancsript tuu bila ya kua na certificate(bachelor dree) ?
na maanisha kwa wale vijana waliomaliza masomo mwaka huu(2018) matokeo tayari ila certificate bado.
mkuu ukiomba utaitwaa Kwa interview lakini wakikuambiaa unyesha original certificate hapo ndo utaumbuka aisee coz ilishawai kutokea jamaa yangu aliitwa Kwa interview then akaishia kuumbuka Kwa kutokuwa na original certificates......asante
 
Haaa kuna organisation nyingi za kimataifa yaan requirement wanatakaga CV na Cover later basi sasa si unaweza kuwadanganya
Kakwambia UTUMISHI na sio hizo za kimataifa mkuu.Jibu utumishi utasumbuka tu utarudishwa siku ya Usaili.
 
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma

July 22, 2014 ·
MASWALI NA MAJIBU YA HOJA MBALIMBALI ZA WADAU
Awali ya yote Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwashukuru wadau wote waliotuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa kipindi chote cha mwezi Mei hadi Julai, 2014. Maswali yao yanasaidia sana pindi yanapotolewa majibu ya jumla kwa faida ya wasomaji wetu wengine katika kuelimishana kuhusu masuala yanayohusu uendeshaji wa mchakato wa ajira Serikalini.
SWALI
1. Nimekuwa mfuatiliaji wa Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo mitandao ya kijamii na kuna wakati niliona baadhi ya wadau wenu wakilalamikia suala la kutumia transcript katika kutuma maombi ya kazi. Je, Sekretarieti ya Ajira mnalizungumziaje suala hilo?
JIBU
Kuhusu suala la matumizi ya “Transcript” katika kuwasilisha maombi ya kazi inakubalika ila kutegemeana na muda wa mhusika aliomaliza masomo/elimu yake. Kwa mfano mhusika amemaliza chuo miaka miwili iliyopita na chuo alichomaliza elimu/mafunzo yake bado hakijatoa vyeti kwa wahitimu wake, basi mwombaji anaweza kutumia transcript kuwasilisha maombi yake ya kazi. Ila endapo mwombaji atatumia transcript kuwasilisha maombi na chuo husika alichomaliza kilishatoa vyeti vya kuhitimu atatakiwa kuambatanisha na nakala ya cheti cha kuhitimu na siku ya usaili anapaswa kuja na nakala halisi zote za taaluma aliyonayo na si kuendelea kutumia transcript peke yake. Aidha, ni muhimu waombaji wakafahamu kuwa endapo cheti cha kuhitimu hakijatoka chuoni na mhusika ameona tangazo na kutuma maombi kwa kuwasilisha transcripts zilizoandikwa provisional, au provisional results hazitakubaliwa.
MWENYE UELEWA NA HILI NAOMBA ANISAIDIE
 
Cha muhimu hapo ni cheti tu,unaweza ukatuma maombi na usiwe 'shortlisted' katika utumishi hakuna blablaa kielelezo cha kuhitimu ni cheti na si matokeo
 
Nina rafkiangu alipata kazi kupitia sektretarieti ya ajira.

Hakuwa na cheti wala transcript alikuwa na statement of results,tena alipangiwa Kwene reputable autonomous government institution kabisa.
Nini nataka kusema?
Mkuu kujaribu ni juu yako na katika kujaribu kuna kujifunza au kufanikiwa,kwahiyo Jaribu mkuu inaweza kuwa bahati yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom