Qaboos: Sultani amefariki, aishi Sultani!

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,239
Pole pole wingu la huzuni lilikunjuka na mbio mbio likatanda na kuigubika Omani nzima na nje yake usiku wa kuamkia Ijumaa, Januari 10, 2020. Nyakati hizo ndipo alipofariki mtawala wa nchi hiyo, Qaboos bin Said bin Taimur al Said kwenye kasri ya Beit al Baraka, Maskati, baada ya kuugua maradhi ya saratani ya tumbo kuanzia 2015. Alikuwa na umri wa miaka 79.

Siku chache za mwisho za uhai wake zilikuwa za mtihani mkubwa kwa aila ya kifalme ya Omani kwani hali ya afya ya Sultan Qaboos ilizidi kuwa mbaya. Inasemekana kwamba mashini ndizo zilizokuwa zikimsaidia aendelee kuishi.

Inasemekana pia kwamba mchakato wa kumteua mrithi wa ufalme ulikamilika kabla ya kutangazwa kifo cha Qaboos. Jina la mrithi aliyetajwa ni lile lile alilokuwa ameliandika mwenyewe Qaboos na lililokuwemo ndani ya bashasha iliyokuwa imefungwa kwa mhuri wake. Lilikuwa la Haitham bin Tariq bin Taimur al Said, mmoja wa binami zake, mwenye umri wa miaka 65.

Haitham anaurithi ufalme akiwa na umri mkubwa ukimlinganisha na Qaboos aliyekuwa na miaka 29 au na baba yake Qaboos, Said bin Taimur aliyekuwa na miaka 22 au na babu yao kina Qaboos na Haitham, Taimur bin Feisal, aliyekuwa na umri wa miaka 27.

Hali kadhalika, sultani huyo mpya ana uzoefu wa muda mrefu wa shughuli za kiserikali hasa katika wizara ya mambo ya nje ambako aliwahi kuwa waziri mdogo (1986-1994) na halafu katibu mkuu wa wizara hiyo (1994-2002).

Alisomea mambo ya utumishi kwenye wizara ya nje katika chuo kikuu cha Oxford mwaka 1979. Mwishowe aliteuliwa waziri wa urathi na utamaduni kuanzia Machi 2002 hadi alipourithi ufalme.

Haitham ni mshabiki wa michezo na katika miaka ya 1980 alikuwa mkuu wa mwanzo wa Jumuiya ya Soka ya Omani.

Kwa muda amekuwa akitajwatajwa kwamba huenda akawa yeye mfalme kwa sababu ikijulikana kwamba Qaboos akimpenda na alikuwa na imani na uwezo wake wa kutawala.

Jambo la murua lililofanyika ni kuifungua moja kwa moja ile bahasha aliyoiacha Qaboos. Ilikuwa sawa na yanayotokea Uingereza mfalme anapofariki. Hutangazwa: “mfalme amefariki, aishi mfalme!” yaani mfalme amefariki dunia lakini Mungu amjaalie umri mrefu huyu mpya.

Kuna maelfu kwa maelfu ya Waomani wasiomjua mtawala mwengine wa taifa lao ila Qaboos. Wengi wakimpenda. Na wengi wakimshukuru yeye binafsi kuwa ndiye aliyewapatia ufanisi walio nao na ndiye aliyelipatia taifa lao heshima miongoni mwa nchi zilizo ndani ya ukanda wa Mashariki ya Kati.

Kuna hata wenye kuupinga mfumo wa utawala wa kifalme waliokuwa wakimsifu kwa uongozi wake.

Qaboos, aliyekuwa sultani wa 14 wa Omani, alikuwa na umahiri wenye kupigiwa mfano. Alikuwa mfalme, mwanajeshi, mkuu wa serikali, msuluhishi wa mizozo ya kimataifa na mwanadiplomasia wa hali ya juu. Zaidi ya yote alikuwa baba wa Omani mpya.

Mfalme huyo alikuwa na nguvu nyingi za kidola na wala taifa lake halijawa la kidemokrasia. Alikuwa sultani, waziri mkuu, amiri jeshi wa majeshi yote, waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya nje na mwenyekiti wa Benki Kuu ya Omani.

Nyadhifa zote hizo alizikusanya mikononi mwake. Yeye ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuwateua majaji.

Ufalme wake ulikuwa ni ufalme kamili usiowekewa mipaka ya kikatiba. Haukuwa ufalme wa kikatiba kama wa Uingereza, kwa mfano. Hakukuwa na mgawanyiko wa madaraka kwa mujibu wa mihimili tofauti ya dola.

Inasemekana kwamba washauri wake wakuu walikuwa kwenye “maktab al qasr” (ofisi ya kasri). Hiyo ni kama wizara iliyo ndani ya kasri ya mfalme na iliyojaa watendaji wenye ushawishi mkubwa katika mambo ya usalama na intelijensia.

Hakuruhusu vyama vya siasa. Upinzani dhidi yake haukuvumiliwa. Waliojaribu kumpindua walichukuliwa hatua kali.

Licha ya yote hayo, wananchi wake wakimpenda kwa dhati. Wakimpenda kwa sababu kwanza akitawala kwa busara, akijizuia asiyatumie vibaya madaraka makubwa na mapana aliyokuwa nayo. Ingawa utawala wake haukuwa wa kidemokrasia lakini sio wengi waliouona kuwa ni utawala uliowakandamiza.

Pili, alijitahidi sana kuyatumia mapato ya nchi yake kwa maendeleo. Sera zake za kukuza elimu na vipaji vya Waomani ziliwasaidia maelfu kwa maelfu ya wanafunzi wapelekwe vyuo vikuu vya nchi za nje ili wachote elimu katika fani mbalimbali. Hivi sasa Omani inajitegemea kwa kiwango kikubwa kwa uwezo wa kielimu wa wananchi wake.

Omani haikuwa iliyoendelea kama ilivyo sasa. Chini ya baba yake, Said bin Tamur, Omani ilikuwa nchi iliyotupwa nyuma kimaendeleo na mataifa karibu yote ya Kiarabu.

Omani ya miaka hiyo ilikuwa Omani iliyojiweka kando isiyotaka maingiliano na mataida mengine. Ilijifunga na ikajifungia ndani yenyewe ikiwaogopa wahamiaji kutoka nje hata wale waliokuwa na asili ya Omani.

Baba yake Qaboos alikuwa na mambo ya kushangaza. Sultani huyo, Said bin Taimur, alikuwa mtu aliyesoma. Baba yake alimpeleka India alikosoma chuo cha Mayo, moja ya vyuo vya kale vya India huko Rajputana na baadaye Baghdad, lakini alipoushika usultani alikuwa akifanya mambo yasiyolingana na elimu pamoja na ujuzi wake.

Alipiga marufuku watu wasicheze soka, wasizungumze hadharani kwa muda ulio zaidi ya dakika 15, wasiendeshe baiskeli, wasiwe na redio, wasivute sigara hadharani, wasivae viatu vya buti, au suruali, wala wasivae miwani za jua,

Huduma za afya na elimu zilikuwa duni. Katika nchi nzima kulikuwa na hospitali moja na skuli tatu za msingi. Hakukuwa na skuli ya sekondari na hizo tatu za msingi mara kwa mara sultani akitishia kuzifunga. Ni asilimia tano tu ya wakaazi wote wa Omani waliokuwa na uwezo wa kuandika na kusoma.

Maisha yalikuwa magumu, magonjwa ya aina kwa aina, mengine ya kutisha, yalisambaa nchini, na vifo vya watoto wachanga vilikuwa vingi mno. Zaidi ya hayo kulikuwa na barabara moja tu ya lami na ilikuwa na urefu wa kilomita 10.

Kifo cha sultani huyo kimeiingiza Omani katika zama mpya. Zama zake yeye zilikuwa ni zama za mabadiliko makubwa yaliyoigeuza nchi yake na kuinyanyua kimaendeleo katika kipindi kifupi.

Qaboos aliitawala Omani kwa muda unaokaribia miaka 50 kuanzia Julai 23, 1970 siku aliyompindua baba yake, Said bin Taimur.

Kwa hakika, mapinduzi hayo yalipikwa jijini London, Uingereza. Wapishi walikuwa Shirika la Ujasusi la Uingereza, MI6, likishirikiana na watumishi wakuu wa wizara za ulinzi na mambo ya nje za Uingereza.

Waziri Mkuu wa siku hizo, Sir Edward Heath, aliyekuwa akiongoza serikali ya chama cha Conservative alitoa idhini mapinduzi hayo yatekelezwe.

Ilikuwa ni miongoni mwa maamuzi ya mwanzo magumu aliyoyakata tangu awe waziri mkuu Juni 19, 1970 ingawa huenda ikawa uamuzi huo wa kumpindua Said bin Taimur ulikatwa na mapema zaidi katika miezi ya mwisho ya kuwa madarakani Harold Wilson, waziri mkuu wa serikali ya chama cha Labour, aliyemtangulia Heath.

Wakati huo Omani ilikuwa imekwishaanza kusafirisha na kuuza mafuta nje ya nchi. Mafuta yaligunduliwa mwanzo nchini humo 1964 na ilibainika mwaka huo kwamba akiba hiyo ya mafuta ni kubwa sana na inaweza kuuzwa nchi za nje.

Mwaka 1976 ndipo Omani ilipoanza kuyauza mafuta yake. Kutoka hapo uchumi wa Omani ukaanza kutegemea sana juu ya mauzo ya mafuta ya petroli.

Mapinduzi ya Qaboos yalikuwa mapinduzi yasiyomwaga damu na yasiyoleta machafuko katika jamii. Badala yake yalisababisha kupatikana kwa neema kubwa. Yaliweza wakati huohuo kuuimarisha utengamano baina ya makabila ya nchi hiyo ambayo zamani yalikuwa hayeshi kuzozana.

Pia yaliikokota Omani na kuitoa kutoka kwenye giza la ujinga na kuiingiza kwenye mwangaza wa maendeleo ya kisasa. Elimu ndiyo msingi alioutumia Qaboos kuijenga Omani mpya. Qaboos alifanikiwa kuyatenda yote aliyoyatenda bila ya kuuhatarisha utamaduni na mila za kijadi za Kiomani.

Katika juhudi zake za kuijenga Omani mpya Qaboos alibahatika kuwa na umati wa Wazanzibari wenye asili ya Kiomani waliosoma na waliokuwa ama wamefukuzwa au waliotoroka Zanzibar baada ya mapinduzi ya 1964. Hasara ya Zanzibar ilikuwa faida kwa Omani.

Jambo la kusikitisha ni kwamba nchi mbili za ukanda wa Afrika Mashariki, Comoro na Zanzibar, zilizokuwa na uhusiano wa muda mrefu na Omani, hazijafanya busara ya kuzitumia vyema fursa ambazo Qaboos binafsi alikuwa tayari kuzipa kwa maendeleo yao.

Jambo moja linalomfanya mtu asite na kulitafakari ni namna Qaboos alivyozikwa. Hapakuwa na mbwembwe kama tunazozishuhudia kwenye mazishi ya viongozi wengine. Na kaburi lake pia ni halikurembwa; ni la kawaida tu kama makaburi ya masultani wa zamani wa Zanzibar.

Chanzo: Raia Mwema

IMG-20200115-WA0025.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
OMANI IMANI AMANI

Nchi hiyo ilishaombewa dua na Mtume wetu S.A.W mpaka leo hii metulia haina vita, tofauti na other countries za kiarabu

Tunamuombea kiongozi mpya Allah amuongoze na amfanyie wepec ktk majukumu yake,,

Muna2penda sana waomani ,nasi watanzania 2nawapenda sana.
 
View attachment 1324340

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitarudi tena shekhe mzigo mrefu huu
 
Back
Top Bottom