Q-NET naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu

Bado mnazidi kutapeliwa ? Mange Kimambi leo amewaanika hao q net na amesema wazi ni matapeli ..jaman watanzania sisi ni mambumbumbu kiasi hiki?
Bora wewe milioni 8, kuna mwingine alikuja humu katapeliwa milioni 10
Kwahiyo unataka kusema Mange ndio amewaanika wakati hii hizi mada zipo humu JF miaka nenda rudi? Kwanza hili bandiko tu la leo limewekwa 12 11hrs, huyo mange kaweka just a few minutes later na katumia picha za humu humu,hivyo hiyo habari kaitoa humu.
 
Mimi mwengewe wife kapigwa 5m. Akanishawishi na mimi kuingia. Nilishtuka mapema sana na nilileta hapa uzi kuhusu hii biashara. Ila mods baadae waliiondoa nadhani kwakuwa kulijitokeza maneno makali kwenye ule uzi

Mpaka sasa wife anaamini yupo sahihi. Na akiona nyuzi hizi anasema sisi hatuielewi qnet.
 
Nenda tu Gamboshi, hiyo hela hupati na mahakamani huwezi shinda maana hawa jamaa wanavibali, wanachokuambia ni wekeza ktk mfumo wa kununua, ukishanunua ujue umeshampa aliyekushawishi kamisheni, sasa ili upate na wewe tafuta fala mwingine umshawishi anunue ili upate kamisheni, product ya million 8 uliyokwishaichukua in a form of purchasing itawezaje kutengeneza hela for you, haiwezekeni..Qnet ideology is to fool someone then train him to fool others to earn money!
 
Mke wako Katoa hiyo helaaa na hajapataa chochotee na Bado anasema yupo sahihi???? Na wew unamchekeaa????? Mna mamilioni nin mzeee au mkeo hiyo hela alihongwaaa!??
 
Pole mkuu. Mimi nishawahi kupelekwa kule na jamaa mmoja hivi nilipofika mikocheni kwa warioba nikakuta kikundi cha watu kiukweli ni kama wapo frastrated hivi wakanizunguka na kujitambulisha nikawa na wacheki tu. Baadae nikaingizwa kwenye chumba nikaanza kupewa darasa. Wanaongea mambo ya kipuuzi nikawa hata siwasikilizi navusha tu.baadae nikambiwa nirudi kesho kuendlea na somo sijarudi wala na niliplan nikatoe taarifa kawe polisi waje wawadake.
Ushauri milion 8 haiwezi hata kuzaa 15 milion kwa mwaka kama unafanya biashara halali
 
Haha mkuu jenerali ulimwengu anaita "kujingishwa "
 
Daaah, pole sana mkuu. Neno lao kubwa la utapeli ni kwamba QNET NI WADHAMINI WA MANCHESTER CITY.
Mimi nilwah kuhudhuria presesentation zao pale magomeni. Ila nashukuru Mungu wamegonga niliona utapeli wao mapema sn.
 
Hawa Jamaa wako Mwenge Karibu na Nakiete.Nimeshahudhuria presentation zao 2 kwa kupelekwa na rafiki yangu.Jamaa ni ving'ang'anizi sana unwaambia hela huna hawataki kuelewa. Hii awam ya 5 Sio mchezo mtu nitoe Milion 4.2!.Biashara halali na ambayo ni ya kisayansi ni Forex Ila kwa wasomi na watu makini tu.
 
yaani kweli unanunua saa 8m kwa kuambiwa utapata B3.3 kweli akili iyo au matope wacha wawapige tu hamna namna
 
Wa Tz ni mazuzu..hivi huwezi kufikiria tu kwa akili ya kawaida ujiulize hiyo 3B return inatoka wapi? Kwanza watu wakifanikiwa huwa hawashirikishi walifanyaje kufikia mafanikio, so ukiona mtu anakulazimisha eti akufanikishe Jua ni utapeli.
 

Hahahah nmeipenda hio ideology yao, na wamewekeza effort kubwa kweli kuwachukulia pesa wapuuzi. Hio million 8 bora angenunua mark x akamshikisha mtu kwa million 10.
 
Tanzania kuna fursa nyingi sana naatapeli pia huona fursa zaidi...hawa jamaa Q net niliwai kula keki na juice yao wakati wanafungua ofisi yao mpya makongo juu...yuko Dada mmoja ni mtumishi wa serikali Kibaha ndo alinipigia Simu na kutaka tufanye biashara niliamua kumsikiliza ,nilishangaa sana hakutaka kuniambia kwenye Simu ni aina gani ya biashara ,yeye akaniambia ntajua nikifika ,nilipofika nilimdharau sana baada ya kuona upuuzi ule ...hakika kuelimika sio vyeti jamani...yule Dada nilikuwa namuona wa maana kumbe hovyo kabisa....toka siku iyo sikurudi tena, mbaya zaidi alinipotezea mood yangu maana nilikuwa nakunywa zangu bia nikaacha kwenda kwenye fursa kumbe udwanzi wa kiwango cha juu kabisa...
Alliance motion wanafunzi wengi sana wa IFM ,st.Joseph wameibiwa kweli kweli ,haya Qnet kuna wafanyakazi wa serikali kibao wamepigwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…