Q Chillah anajua mziki, mziki wake hauchoshi

MTINGIJOLI

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
1,358
1,324
Leo nimeamka na mood, ya kusikiliza mziki mzuri, basi katika kusikiliza kwangu nikajikuta namsikiliza huyu gwiji wa Bongo fleva Q Chillah {Q Chief] jamani jamaa anajua, hachoshi masikioni mwako.

Tangu anaanza mziki hadi alipo sasa hivi, namsikiliza hadi machozi yanataka kunitoka, kama hii nyimbo yake inaitwa maua, ni nzuri balaa ila kwenye vituo vya radio sijawahi kuisikia, sijui kama wanayo.

Cha kusikitissha Q Chillah hayupo kwenye ramani ya mziki kabisa, nyimbo za ajabu ajabu ndio zinapata air time na ndio zinatamba, kweli Mungu akunyime vyote lakini asikunyime bahati.

Unaweza upo vizuri lakini huonekani, hakuna hata mmoja anaekutazama, hiki ndio kinachomkuta huyu ndugu yetu leo hii, ila level zake ni nyingine kabisa.
 
Kuna ile albamu yake ina nyimbo kama sexy, marimu aisee jamaa kajaaliwa kipaji ila staili ya maisha imempoteza na kumtoa kwenye reli
 
Wakuu kuna wimbo wake una mashairi haya(its so hard to say goodbye to the woman you love)anayejua jina la huu wimbo tafadhali anisaidie nautafuta sana aisee..
 
Mauaaaaaa sema ndioooooo
Mauaaaa itikia wito waaaaangu
No one like youuuuu
Niliapa kwa Mungu Maua sitokuacha mpenzi....

Hatari sana huu wimbo Na wala hauchoshi
 
Umemsikiliza Q chillah machozi yamekutoka, je ungemsikiliza R kelly, si ungizimia. Sikiliza mziki una time frame yaani zamu zamu, zamu yako ikiisha anakuja mwengine Q chillah si msanii mbaya bali zamu yake ishaisha, aache kulialia kosa kalifanya mwenyewe kushindwa kuwekeza na hata hawa unaowaona wanavuma sasa hivi, mwisho wa siku nao wataporomoka hata wapewe promo kila sekunde watashuka, mziki ndio upo hivyo.
 
Mauaaaaaa sema ndioooooo
Mauaaaa itikia wito waaaaangu
No one like youuuuu
Niliapa kwa Mungu Maua sitokuacha mpenzi....

Hatari sana huu wimbo Na wala hauchoshi
Hatari Sana Hii Kitu Kaka, Ameimba Mno Humu
 
Huyu jamaa alinichekesha Sana kuhusu mkataba wa maisha alioingia na promota wake,
Hadi familia ikaingilia Kati kutaka kuuvunja, sijui wamefikia wapi
 
Mkuu sikiliza na kipande kingine cha wimbo wake kinaitwa..watu na maisha yao...nafikiri hajautoa rasmi nao ni mzuri sana.
 
Back
Top Bottom