real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Pwani. Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa watu watatu wakazi wa kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti wanadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo.
Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu amesema ameliagiza jeshi la Polisi wilayani hapa kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.
Tutaendelea kukuletea habari zaidi kuhusu tukio hili.
=> Mwendelezo...
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema kwa taarifa alizonazo, watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati, Kibiti, kisha waliofanya uhalifu huo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao.
Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo.
Lakini akizungumza na Mwananchi leo asubuhi, Kamanda Lyanga amesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risasi na wahalifu kutokomea nao kusikojulikana.
“Tunaendelea na uchunguzi.” Amesema Kamanda Lyanga
Chanzo: Mwananchi
=====
Kwa hizi siku za karibuni, Mkoa wa Pwani umekuwa ukikumbwa na Matukio ya Mauaji ya Mara kwa Mara. Serikali iliangalie hili jambo kwa jicho la pekee sababu watu wasio na hatia wamekuwa wakipoteza Maisha. Hapa chini ni baadhi tu ya Matukio yaliyoripotiwa ya Mauaji kutoka Sehemu tofauti katika Mkoa wa Pwani;
Kibiti, Pwani: Majambazi yaua Askari Polisi NANE(8)
PWANI: Majambazi 4 wameuawa katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi
Mwenyekiti wa kijiji atekwa Ikwiriri, mwingine aokotwa mtoni amefariki kwa jeraha la risasi
KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi
KIBITI: Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mtunda auawa kwa kupigwa risasi
Katibu wa CCM Kata Ya Bungu, Kibiti auawa kwa kupigwa risasi
Polisi waua watatu "wanaodhaniwa' kuua askari Kibiti. Hii kuua watu kwa kudhani mpaka lini?
KIBITI: Watu watatu wameuawa akiwemo Afisa wa Upelelezi (OCCID)
RUFIJI: Mwenyekiti wa kijiji anusurika kuuawa na majambazi
Mwenyekiti wa CCM Rufiji apigwa risasi na kufariki dunia
Rufiji: Mwenyekiti kitongoji cha Kifuru auawa kwa kupigwa risasi
Majambazi yavamia kituo na kuua polisi wawili Ikwiriri Rufiji
Pwani: Mwingine apigwa risasi mchana huu Mkuranga
Mkuranga: Mtendaji wa Kijiji cha Mjawa, mwanakijiji mmoja wauawa
Mauaji Mkuranga: Dereva wa bodaboda akatwa mapanga na kufariki
Majambazi wavamia NMB Mkuranga, Waua Polisi
Askari mwingine auwawa Mkuranga!
Majambazi yaua askari Mkuranga na kujeruhi!
News Alert: - KIBITI: Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi wauawa kwa kupigwa risasi
Pwani: Askari Wawili wa Usalama Barabarani wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti
Na kadharika.