esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi.
Aidha watuhumiwa hao wanadaiwa kukutwa na simu 13 za tochi na smart 4 na laini 22 za kampuni mbalimbali pamoja na orodha ya namba ambazo wanadhaniwa kuwa walitaka kuwatapeli na waliowatapeli.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 13, mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kata ya Zinga, tarafa ya Yombo wilayani Bagamoyo
kupoteza muda wa kujibu ni kumkomoa huyo mwizi (ambaye kwake majibu kama hayo ni cost of doing business..) au kupoteza muda wako na sms yako ?Afadhali, juzi eti wamenitumia hako ka meseji ka hovyo saa kumi ya usiku,........ Nilichomjibu yule tapeli ataenda simulia wenzie
Halafu mengi yanatumia mtandao wa Voda,
Huwa hawana muda wa kusoma sms.kupoteza muda wa kujibu ni kumkomoa huyo mwizi (ambaye kwake majibu kama hayo ni cost of doing business..) au kupoteza muda wako na sms yako ?
Exactly my point..., kuwajibu ni kupoteza muda wako.., yaani wanakuwa wamefanikiwa kuiba sekunde za muda wako...Huwa hawana muda wa kusoma sms.
Wao wakishatupia ndoano majini, wanasubiri chambo kicheze wavute. Hata ukiwapigia muda wa kukujibu hawana. Ogopa sn tapeli.