PWANI: Kiwanda cha nondo kuiingizia Serikali bilioni 200 za kodi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
kiluwa.jpg

Serikali inatarajia kukusanya sh.bilioni 200 kwa mwaka, ikiwa ni mapato ya kodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kimataifa cha Kiluwa Steel Group kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,000 za nondo kwa siku.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa kwa kushirikiana na Wachina, inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwaka huu ambapo fedha hizo zitapatikana baada ya kukamilika awamu tatu za ujenzi wake.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetembelea kiwanda hichoMkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mohammed Kiluwa alisema ujenzi huo utasaidia kuimarisha uchumi.

Kiluwa alisema, awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu, ambapo awamu ya tatu itakamilika Februari mwakani. Kikikamilika, kinatarajiwa kuajiri vijana zaidi ya 500 wa Kitanzania.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa cha kwanza kinachojengwa na mwekezaji mzawa.

Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho katika eneo la Disunyara, Mlandizi mkoani Pwani, utawezesha kuboresha hali ya uchumi kwa wakazi wa eneo hilo na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu alitolea mfano kwa wakazi wa Mtwara, ambao wamenufaika kutokana na ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote ambapo awali walikuwa wakinunua saruji kwa sh.17,000, lakini hivi sasa wanainunua kwa sh. 7,000.

Chanzo: ITV
 
Mi naomba serikali ihakikishe hizo awamu zote zinakamilika isije ikawa maneno tu. Pia kwa anayejua huyu Kiluwa ndio yule aliyemtunza mtoto wake cheni ya gharama sana alipomfanyia birthday yake.
 
Nachangia mada hii katika maeneo mawili kuhusu mkoa wa Mtwara
Kwanza nafikiri pamoja na ukweli kuwa Saruji Mtwara imeshuka bei lakini siyo kwa kiwango cha chini kufikia Tsh 7000.

Lakini kuhusu hicho kiwanda cha Nondo, huyu Mohammed Kiluwa ni Mzawa kabisa wa Mtwara na kifikra yupo vizuri. Hongera yake Mr Kilua angalau umethubutu!
 
Mi naomba serikali ihakikishe hizo awamu zote zinakamilika isije ikawa maneno tu. Pia kwa anayejua huyu Kiluwa ndio yule aliyemtunza mtoto wake cheni ya gharama sana alipomfanyia birthday yake.

Kiluwa tapeli huyo.. Ni mbia na kina Rizwani
 
Nachangia mada hii katika maeneo mawili kuhusu mkoa wa Mtwara
Kwanza nafikiri pamoja na ukweli kuwa Saruji Mtwara imeshuka bei lakini siyo kwa kiwango cha chini kufikia Tsh 7000.

Lakini kuhusu hicho kiwanda cha Nondo, huyu Mohammed Kiluwa ni Mzawa kabisa wa Mtwara na kifikra yupo vizuri. Hongera yake Mr Kilua angalau umethubutu!

Alitapeli viwanja vya KAUMU kule Mtwara.. Tapeli huyo na hicho kiwanda kitakuwa ni cha Rizwani mbia wake
 
Gazeti La Nipache la leo tarehe 14 July, 2016 limeripoti kwamba; Serikali inatarajia kukusanya shilingi bilioni 200 kwa mwaka ikiwa ni mapato ya kodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kimataifa cha Kiluwa Steel Group kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha Tani 3000 za Nondo kwa siku …..

Hongera JK,matunda yako ya safari za nje yanaanza kuonekana sasa.
 
Back
Top Bottom