DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,152
Rais wa Urusi Vladimir Putin, hatohudhuria mkutano wa kilele wa mataifa ya BRICS utakaofanyika Julai 6–7 nchini Brazil, kutokana na hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na taarifa hiyo imethibitishwa na mshauri wa sera za kigeni wa Kremlin, Yuri Ushakov, aliyesema kuwa Putin atashiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao (video link).
Mahakama ya ICC ilitoa hati hiyo mwaka 2023 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Urusi kuanzisha uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya Ukraine vilevile Putin anatuhumiwa na mahakama hiyo kwa kosa la kivita la kuwahamisha mamia ya Watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi hata hivyo Urusi imekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa haitambui mamlaka ya ICC kwani haijasaini mkataba wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Licha ya msimamo huo wa Urusi, hati hiyo ya kukamatwa imekuwa kikwazo kwa Putin kuhudhuria mikutano ya kimataifa inayofanyika katika nchi wanachama wa ICC n mwaka 2023 alijiondoa kuhudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini kwa sababu hiyo hiyo.
Kwa mujibu wa Ushakov, kutoshiriki kwa Putin moja kwa moja katika mkutano wa Brazil kunatokana na changamoto fulani zinazohusiana na masharti ya ICC ambapo serikali ya Brazil haikuweza kutoa msimamo wa wazi wa kumhakikishia usalama wake endapo angesafiri hivyo kwa mara nyingine Urusi imechagua njia ya mtandao kama mbadala wa ushiriki wake.