Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

Bro umenena vema naomba unitafute kwa namba hii 0744312003 nahitaji msada ktk hili

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Sijasoma yote ila binafsi nashauri ukishindwa kabisa kuacha basi kunywa beer tu...
Makali ( whiskey, cogniac, vodka, gin) achana nazo
 
Sijakunywa pombe yoyote tangu kunywa Champagne ya kusheherekea mwaka mpya January 1 2024.

Licha ya kwamba nina Scotch, Vodka, Tequila, wine na beer ndani.
 
Sijakunywa pombe yoyote tangu kunywa Champagne ya kusheherekea mwaka mpya January 1 2024.

Licha ya kwamba nina Scotch, Vodka, Tequila, wine na beer ndani.
Wewe unaweza kuacha kabisa, kwasababu unazo na hazikusumbui. Wengi huacha wakiishiwa, wakipata wanaendelea.
Sasa unapaswa kuziweka kwa ajili ya wageni tu au zigawe kabisa ili uwe mwanzo wa kuacha kabisa.
 
Kwenye madhara ya pombe nadhani kikubwa ni kipato, ungejikita hapo, NI kweli Sisi watu wa watu pombe inatugharimu Sana pesa.

Unakunywa pombe ya sh 10,000/= lakini unalipa bill ya 100,000/= Kwa sababu ya wandewa, na wewe huwa wanakutowa vilevile.

Kwenye maradhi sasa hivi mpaka vyakula vimejaa maradhi.

Hamasisha watu kutumia Alkaline Kwa wingi badala ya kuwatisha na madhara ya pombe.

Haya maisha yalivyokaa bila pombe unaweza ukadata ukawa kichaa bure.
 
Sijakunywa pombe yoyote tangu kunywa Champagne ya kusheherekea mwaka mpya January 1 2024.

Licha ya kwamba nina Scotch, Vodka, Tequila, wine na beer ndani.
Africa hatunywi pombe kama starehe watu wengi hawajui huu ukweli.

Hakuna starehe ya kunywa bia kreti moja mtu mmoja, mkae mkijuwa kuna Vitu watu vinawasumbuwa.

Hata Yule Gardner G Habash inasemekana pombe Kali ndio source ya ugonjwa wake.

Sasa jiulize mtu asiye na stress atamaliza Vipi chupa zima la scotch?

Labda ninachotaka kusema hapa kama ilivyo tatizo la vidonda vya tumbo sababu yake kuu ni kuishi dunia ya tatu, basi na issue ya pombe iko hivyohivyo.

Bongo sasa hivi ni 03:38 midnight lakini nasikia mziki kwenye pub ya Jirani watu wanakula maji tena asubuhi tunaamkia working day? Unadhani ni kweli hawa watu Wana furaha?

Wengine wakirudi nyumbani mapema ni kama Jehenamu wake zao Wana midomo kama chuchunge nyumbani hapakaliki.
 
Wewe unaweza kuacha kabisa, kwasababu unazo na hazikusumbui. Wengi huacha wakiishiwa, wakipata wanaendelea.
Sasa unapaswa kuziweka kwa ajili ya wageni tu au zigawe kabisa ili uwe mwanzo wa kuacha kabisa.
Si mara ya kwanza, nishaacha kwa miaka miwili straight, mara mbili. Ila safari hii naweza kuacha kabisa.

Hizo za wageni haziwezi kukosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…