Pumzikeni kwa amani

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
1,383
Reaction score
2,587
Hakuna aliyejua kuwa siku ile ingekuwa ndio mwisho wa maisha yake. Kifo ni fumbo kubwa sana kwa mwanadamu nani ajuaye siku ya kuondoka kwake? hakuna ajuaye.

Mngekuwa mnajua kuwa meli ile itapinduka mda mfupi kabla ya kutia nanga hakuna ambaye angekubali kupanda meli ile. Mmekufa kifo cha uchungu mkubwa. Mlikunywa maji mengi kupita kiasi ,mkakosa hewa ya oksijeni hadi mauti ikawakuta. Najua mlijaribu kujitetea ili muokoe maisha yenu, mlijaribu kupiga kelele ili tuwasadie ,lakini hakuna aliyekuja kuwasadia. Wapendwa naomba mtusamehe sana tulichelewa kufika ,tulitamani sana tuwasaidie lakini hatukuweza.

Tazama leo mmezikwa kwa mamia. Mmezikwa sehemu moja bila kupenda. Ndoto zenu zimekati ghafla,zimezima kama mwanga wa mshumaa. Mmeacha uchungu mkali kwa famiia zenu.Taifa linalia ,Watanzania wanaombleza hakuna wa kuwafariji.

Tunawaombea kwa Mungu ili roho zenu zipumzike kwa amani milele na milele . Mmetangulia ila iko siku moja tutaonana tena. Nawaomba huko mliko muendelee kuiombea nchi yetu ili iepukane na majanga kama haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…