Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Mimi nilistaafu utumishi wa serikali tangu June 2015. Hadi leo bado nasumbuliwa juu ya kulipwa mafao yangu.
Pamoja na kufuatilia makao makuu ya PSPF Dsm majibu ambayo nimekuwa nikipewa ni kwamba serikali bado haijawasilisha michango yake.
Kinachonikera ni kwamba maisha ni magumu nashindwa hata kulipia ada ya shule ya watoto wangu pamoja na huduma nyingine muhimu za kijamii.
Ule utaratibu uliokuwepo miaka ya nyuma wa kuwasumbua wastaafu juu ya kulipwa mafao yao hadi kupelekea wengine kufariki dunia bila kulipwa dalili zinaonyesha usumbufu huo umerejea ktk mfuko huo.
Ikumbukwe kuwa kabla ya kustaafu, mstaafu anatoa notisi miezi sita kabla ili taratibu ziandaliwe na unapofika muda wa kuagana na mwajiri wake anakabidhiwa chake.
PSPF tuelezeni iwapo pesa hizi mnazifanyia biashara au ugumu uko wapi. Kama kweli maelezo tunayopewa kuwa serikali haijapeleka michango yake ni ya kweli basi namuomba waziri wa fedha atimize wajibu wake ktk hili.
Serikali inapotujali wakati tunaitumikia basi itujali pia unapofika muda wa kuagana kwa kutulipa kwa wakati. Hali ni mbaya Mkurugenzi wa PSPF timiza majukumu yako usije ukatumbuliwa jipu.