Propaganda na ugandizi wa mbeba maono wa CHADEMA

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Posts
403
Reaction score
211
Katika kuendeleza propaganda za safari ya matumaini; mbeba maono wa CHADEMA katika uchaguzi wa 2015 alituaminisha watanzania kuwa tukapige kura ushindi tumwachie yeye.

Kilichotokea akaangukia pua na kutuambia hatambui matokeo ila tuwe na subira. Subira imekuwa subiri. Katika ufunguzi wa kampeni za marudio Kinondoni; mbeba maono huyo kaja na propaganda inayopingana na ile ya 2015 akituamisha vijana tusilale na kusisitiza kulinda kura.

Hizi propaganda za mbeba maono wa CHADEMA ni ishara tosha ya kufeli katika uchaguzi wa marudio. Yani siku ya kwanza ya ufunguzi wa kampeni hujajua upepo upoje unaleta propaganda za ujima. Kwa propaganda hizi; tusubiri kipigo cha mbwa mwitu.

Watu wanataka sera zitakazotatua changamoto za Kinondoni si kulinda kura ambacho ni kitendo cha mwisho baada ya kutathmini umepata ushawishi mkubwa na unatarajia kushinda na unaona kunadalili za figisufigisu.

Naona chombo kinaenda kuzama. Dalili za visingizio vimeanza asubuhi.
 
Kwahiyo ww katika hotuba yake nzima amezungumzia kulinda kura tuu
 
hao ndio chadema wa sasa badala ya kujibu hoja wanakimbilia kutukana ndio maana kila siku wanaishia kupelekwa mahakamani jifunzeni kubishana kwa hoja
 
Haya warinde kura, maana CCM in wezi wakura.je yakitokea Yale ya Mwaka 2015 ambayo Hamiri jeshi alipo Sema kule Mwanza kuwa" mm nasema kama hamiri jeshi kila mtu akimaliza kupiga kura arudi nyumbani" je mtalinda kura?
 
Katika kuendeleza propaganda za safari ya matumaini; mbeba maono wa CHADEMA katika uchaguzi wa 2015 alituaminisha watanzania kuwa tukapige kura ushindi tumwachie yeye.

Kilichotokea akaangukia pua na kutuambia hatambui matokeo ila tuwe na subira. Subira imekuwa subiri. Katika ufunguzi wa kampeni za marudio Kinondoni; mbeba maono huyo kaja na propaganda inayopingana na ile ya 2015 akituamisha vijana tusilale na kusisitiza kulinda kura.

Hizi propaganda za mbeba maono wa CHADEMA ni ishara tosha ya kufeli katika uchaguzi wa marudio. Yani siku ya kwanza ya ufunguzi wa kampeni hujajua upepo upoje unaleta propaganda za ujima. Kwa propaganda hizi; tusubiri kipigo cha mbwa mwitu.

Watu wanataka sera zitakazotatua changamoto za Kinondoni si kulinda kura ambacho ni kitendo cha mwisho baada ya kutathmini umepata ushawishi mkubwa na unatarajia kushinda na unaona kunadalili za figisufigisu.

Naona chombo kinaenda kuzama. Dalili za visingizio vimeanza asubuhi.

Hivi kuna chama umewahi kusikia kikifanya kampeni kikasema tutashindwa uchaguzi?Duh Pole sana.Hata Mgonjwa akiwa hospitalini huwa hasemi nakufa kesho.

Mmetabiria Chadema iko ICU sasa pressure ya nini??
 
Back
Top Bottom