Pronunciation hii mmmh ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pronunciation hii mmmh !

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Judgement, Feb 10, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Halow ! My fellow Jf Membars.
  THE PRODUCTION OF THE SOUND OF SPEECH .
  Niko katika cafeteria maarufu hapa mjini.
  Nimeingia humu kwa shabaha ya kupata ka'gilasi ka'Juice na vijibajia viwili-vitatu then nichape lapa na mishimishe zangu.
  Pembeni yangu meza jirani nimewakuta wadada wa3 , madada ambao wanaongea sana kuliko ya kilichowapeleka pale (kula na kunywa).
  Kwakua mi katika meza yangu, sikua na waku'share nae, hivyo hao wadada ndiyo wakawa Redio, Tv yangu.
  Nikamsikia mmojawao akisema ;-
  "Aisey yule mkaka mnajua keshaniangukia sana !
  Alafu yule mkaka yuko lisonable (Resonable) sana!
  Ukimdipu (ukim'beep) tu anakupigia, tena kila siku razima (lazima) anitumie cledit (credit) .
  Tena hana hasila (hasira) sevelo times (several) mkaka ni mtu wa smire (smile) .
  In short kwangu mie japo si muingereza lakini uongeaji huu hua unatia kichefuchefu kupita sana.
  Hapa majukwaani Jf tatizo hili pia limeshamiri so many membars wanajeruhi lugha zote tunazozitumia hapa, lakini membars ama wanafumbiana macho ama wanaoneana aibu kukosoana na kurekibishana mimi sijui.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,952
  Likes Received: 5,095
  Trophy Points: 280

  hata wewe hapo juu umechemka.

  Ila inakera sana 'l' na 'r' zinapotumika sivyo. Au kwenye 'm' inawekwa 'mu'

  sema inabidi kupotezea kuna makabila hayana 'l' na 'r' au wanatumie ndivyo sivyo.

  Lakini kazi inakuwa pale mtu anapolazimisha kiingereza wakati kiswahili tu mgogoro.
   
 3. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,003
  Likes Received: 1,884
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa vizuri hapo walikuwa wanazungumza kwa maandishi au?maana ulichokiandika ni cha kimaandishi zaidi.
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa kunirekibisha namie, hivyo ndivyo tutakavyomudu kuelimishana. Tukipotezeana tutaendelea kudumaza, capacity za uelewa wetu.
   
 5. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,374
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  ha ha haaaaaaa, huku kwetu Znz kuna company 1 inaitwa brac basi kuna dada m1 alikua ananiulizia ilipo kwa kutamka blac badala ya brac, It took me ages to understand her mana mi nljua anakusudia black colour
   
 6. F

  FEELINGS Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mawazo yako ni mazuri sana. Lakini lazima ujue kwa mzungumzaji ambaye lugha anayozungumza si lugha yake ya kwanza (lugha mama) mara nyingi tegemea ataijeruhi. Kimsingi si vema kutumia lugha usiyokuwa na umilisi nayo hasa kama muktadha haulazimishi kutumia lugha hiyo. Kwa mafano ndugu yangu angalia kosa ulilolitenda: Umeandika "... So many membars..." badala ya "...so many members...". hivyo wakati mwingine tunawapotezea tu kwasababu ujumbe wanaokusudia unakuwa umefika.
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nimekuelewa mkuu, but kuna spell error (kama ulioitoa kwangu) na kuna pronunciation error ! Hizi writin' error hazikeri sana (kero yake ni minor)
  error za matamshi kimimi ndiyo hunipa kichefchef.
   
 8. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ebu cheki na wewe huko
  Membars au members? Members haina 'a' wewe, na wewe ni mshamba kama hao wadada wako tu. Jipange sawa sawa
   
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,305
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo tupronounce kama nani?kumbaf kabisa mie mbantu sirembi bwn kwetu hakuna 'l' kuna 'r' na kama hutaki kaa kimya.nakwenda kurara mura
   
 10. pinkmousse

  pinkmousse JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili ni tatizo sugu,hata baadhi ya watangazaji wa siku hizi wa redio na tv utasikia wanatamka visivyo,tusaidiane tu kurekebishana ingawa baadhi ya watu hawapendi wanasema hawawezi kubadilika kwa sababu tangu utotoni wanaongea hivyo.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mh. Mi-hasira yote ya nini ? Hata hivyo wengi wanaokwenda lala na mihasira ni wale wanaolala peke yao, mwenza kwishney !
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,575
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  nimekupata mkuu.
  Kuhusu 'r' na 'l' kweli ni makosa, isipokuwa kwa baadhi ya maneno ambayo yana dialectal multi pronounciation, au alofoni za kilahaja, mfano 'kulamba' na 'kuramba'.
  Kuhusu 'm' na 'mu', wala hakuna makosa hapo, hicho ni Kiswahili fasaha, hasa lahaja za pwani ya Afrika Mashariki na lahaja ya Kingwana inayopatika Mashariki mwa Kongo.
  Note tafauti kati ya usanifu na ufasaha, lugha inaweza kuwa fasaha lakini isiwe sanifu.
   
 13. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 7,997
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Asante judgement kwa kunisaidia maana hata mimi nilikuwa na wazo la kuanzisha thread kuhusu matumizii ya 'l' na 'r' hasa hapa JF. Wapo wanaJF wanaandika 'amli' badala ya 'amri' 'fulaha' badala ya 'furaha' nk. kiasi kwamba napata wazo pengine wanaJF wengi wanatoka mikoa ya Tabora, Shinyanga, na kanda ya ziwa victoria kwa sababu wenyeji wa maeneo haya huchanganya sana 'l' na 'r'

  Ila iwapo mtu ni msomi, inatakiwa uwe mwangalifu kwenye mtego huu.Kinachonishangaza na kunikera ni hizo herufi mbili kutumika visivyo HAPA JF! Tuitendee lugha yetu ya Kiswahili haki.
   
Loading...