Okoa Hip Hop ni harakati maalumu zilizoanzishwa mwishoni wa mwaka 2007 baada ya kilio cha mashabiki wa hip hop kuhusu kudidimia kwa muziki huo pendwa. Project hii ilijumuisha wasanii kama Salu-T, Saigon, Magazijuto, Fid Q, Nako 2 Nako, Geez Mabovu (R.I.P), Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Jay Moe, Adili , Mapacha, Blac, Langa (R.I.P), n.k
ADILI a.k.a HISABATI ndie founder wa platform hii, madhumuni ya idea yake hii ilikuwa ni kupigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama ilivyo katika aina zingine za muziki hapa bongo. Pia ni kuhakikisha kila msanii (washiriki) anapata nafasi ya kupromote kazi zake kupitia platform iyo, maana watu waliohudhuria harakati izo waliweza kujipatia bidhaa za wasanii wa hip hop waliomo katika mradi huo iwe ni tapes, tshirt, cd, n.k
Sababu kuu ya project hiyo ilikuwa ni KUIOKOA hip hop kabla haijapotea kabisa in Tanzania community. Ni kupigana na mnyonyaji mkuu wa muziki huu bongo ili kuiweka HIP HOP kwenye hadhi yake inayostahili kuwepo.
MNYONYAJI mkuu ni MUSIC INDUSTRY nzima, in particular the MEDIA. Mnyonyaji huyu ameshaweka mikakati makini sana kuhakikisha kwamba hip hop haifanyi vizuri kabisa bongo. Katika moja ya Interview za gwiji Adili mwanaHisabati, aliwahi kusema hivi: Iwapo hatutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunafanya hizi harakati, kweli kabisa hip hop itapotea na kutakuwa hakuna wa kuikoa kwani sisi wanahip hop ndio wa kuiokoa, no one else
Katika PROJECT hii, mambo mengi yalifanyika, ikiwa ni pamoja na kutoa documentary ambayo inaelezea historia nzima ya Hip hop ya bongo, pia documentary hii ilijumuisha exclusive videos za wasanii washiriki. Documentary hii iliwahi kuoneshwa pia kwenye tamasha la USIKU WA HIP-HOP (HIP HOP NIGHT) pale Dar Live Mbagala, mwezi March 2012.
In short, OKOA HIP HOP ilikuwa ni harakati za kuleta mapinduzi ya kuhakikisha kwamba wasanii wa hip hop wanaungana katika kupigania haki zao na muziki huu. Harakati hizi zilifanyika kwa tour mbali mbali mikoani.
NOW, Back to the concern ya mleta uzi: Je ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hujuma hizi za kuuhujumu (sarbotage) huu muziki hadi wasanii hawa kuamua kuanzisha hatua za makusudi kuuokoa?
RESPONSE: kumbuka vizuri harakati za ANTI-VIRUS and its primary 'target', then jibu la swali lako utalipata. ANTI-VIRUS movements ilikuwa ni muendelezo wa OKOA HIP HOP movements. Thus, harakati za anti-virus project zilikuwa ni 'next episode' ya okoa hip hop project with the same theme, same target, same objectives, same goal, but with different strategies.
Hopefully mchango wangu umekupa mwanga kidogo japo pa kuanzia.
-Kaveli-