Project 'OKOA HIP HOP' ililenga nini ?

Project 'OKOA HIP HOP' ililenga nini ?

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
Habari wadau,

Naomba kuleta hii hoja kwenu tuijadili/munifumbue macho kidogo. Hii inahusu moja ya project kubwa za kimuziki zilizowahi kufanyika inaitwa 'OKOA HIP HOP'

Hii ni project kubwa iliyowahi kufanyika ikiwahusisha wasanii wote wa Hip Hop na kama nakumbuka vizuri walizunguka mikoa kadhaa ikiwemo Dar es Salaam na Arusha na wasanii nnaokumbuka haraka haraka waliozunguka ktk project hii ni Kala Pina na Kikosi cha mizinga, Nako 2 Nako soldiers, River Camp Soldiers, Chid benz, Ditto, Fid Q, Mapacha, Langa (R.I.P), Geez Mabovu (R.I.P) na wengineo wengi.

Sasa mimi hoja yangu iko hapa kuwa; kulingana na slogan ya project ilivyokuwa inasema Okoa Hip Hop maana yake ilikuwa ni harakati mahususi kwa ajili ya kuokoa muziki wa hip hop kutoka ktk hatari ya kupotea/kupotezwa. Inasemekana project hii ilikuja mahususi baada ya kuwepo kwa njama za makusudi za kuupoteza muziki huu wa hip hop.

Je ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hujuma hizi za kuuhujumu (sarbotage) huu muziki hadi wasanii hawa kuamua kuanzisha hatua za makusudi kuuokoa? Na hujuma zilikuwa za namna gani? Michango yenu itanipa uelewa mkubwa sana ktk hili.

Asanteni nawasilisha.
 
Ngoja aje Kaveli atakuwa na majibu mazuri zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Okoa Hip Hop ni harakati maalumu zilizoanzishwa mwishoni wa mwaka 2007 baada ya kilio cha mashabiki wa hip hop kuhusu kudidimia kwa muziki huo pendwa. Project hii ilijumuisha wasanii kama Salu-T, Saigon, Magazijuto, Fid Q, Nako 2 Nako, Geez Mabovu (R.I.P), Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Jay Moe, Adili , Mapacha, Blac, Langa (R.I.P), n.k

ADILI a.k.a HISABATI ndie founder wa platform hii, madhumuni ya idea yake hii ilikuwa ni kupigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama ilivyo katika aina zingine za muziki hapa bongo. Pia ni kuhakikisha kila msanii (washiriki) anapata nafasi ya kupromote kazi zake kupitia platform iyo, maana watu waliohudhuria harakati izo waliweza kujipatia bidhaa za wasanii wa hip hop waliomo katika mradi huo iwe ni tapes, tshirt, cd, n.k

Sababu kuu ya project hiyo ilikuwa ni KUIOKOA hip hop kabla haijapotea kabisa in Tanzania community. Ni kupigana na mnyonyaji mkuu wa muziki huu bongo ili kuiweka HIP HOP kwenye hadhi yake inayostahili kuwepo.

MNYONYAJI mkuu ni MUSIC INDUSTRY nzima, in particular the MEDIA. Mnyonyaji huyu ameshaweka mikakati makini sana kuhakikisha kwamba hip hop haifanyi vizuri kabisa bongo. Katika moja ya Interview za gwiji Adili mwanaHisabati, aliwahi kusema hivi: "Iwapo hatutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunafanya hizi harakati, kweli kabisa hip hop itapotea na kutakuwa hakuna wa kuikoa kwani sisi wanahip hop ndio wa kuiokoa, no one else"

Katika PROJECT hii, mambo mengi yalifanyika, ikiwa ni pamoja na kutoa documentary ambayo inaelezea historia nzima ya Hip hop ya bongo, pia documentary hii ilijumuisha exclusive videos za wasanii washiriki. Documentary hii iliwahi kuoneshwa pia kwenye tamasha la USIKU WA HIP-HOP (HIP HOP NIGHT) pale Dar Live Mbagala, mwezi March 2012.

In short, OKOA HIP HOP ilikuwa ni harakati za kuleta mapinduzi ya kuhakikisha kwamba wasanii wa hip hop wanaungana katika kupigania haki zao na muziki huu. Harakati hizi zilifanyika kwa tour mbali mbali mikoani.

NOW, Back to the concern ya mleta uzi: Je ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hujuma hizi za kuuhujumu (sarbotage) huu muziki hadi wasanii hawa kuamua kuanzisha hatua za makusudi kuuokoa?

RESPONSE: kumbuka vizuri harakati za ANTI-VIRUS and its primary 'target', then jibu la swali lako utalipata. ANTI-VIRUS movements ilikuwa ni muendelezo wa OKOA HIP HOP movements. Thus, harakati za anti-virus project zilikuwa ni 'next episode' ya okoa hip hop project with the same theme, same target, same objectives, same goal, but with different strategies.

Hopefully mchango wangu umekupa mwanga kidogo japo pa kuanzia.

-Kaveli-
 
Kaveli

Asante sana Kaveli umejibu vizuri sana, nimeridhika. Umegusa hata angle ambazo nilikuwa nimezisahau ktk hoja yangu.

Kuhusu ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hizi 'sarbotage' na mimi pia nilikuwa nahisi hao hao ulionitajia kwa kificho (ambao ANTI VIRUS imewachana kwa uwazi zaidi), nimepata uelewa mpana zaidi kwa mchango wako huu kiongozi.

Akina LIKUD karibuni tupate na mchango wenu hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kaveli

mkuu kaveli hivi hii ilikua sambamba na ile hiphop summit ya sugu?
 
Last edited by a moderator:
Kaveli

mkuu kaveli hivi hii ilikua sambamba na ile hiphop summit ya sugu?

Tanzania Hip Hop Summit ya Sugu lilikuwa ni kongamano lenye lengo la kuwakutanisha wasanii na wadau wa muziki wa hip hop kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali juu ya ustawi wa muziki wa hip-hop sambamba na mustakabali wao. Summit hii ilikuwa primarily planned iwe inafanyika mara 1 tu kila mwaka (yaani 'annual'), na summit ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 kama nakumbuka vizuri.

So naweza kukujibu kwamba YES harakati za 'OKOA HIP HOP' ilikuwa zinaenda sambamba (ideally) na Tanzania Hip Hop Summit ya Sugu, kwani movements zote hizi mbili zililenga kitu kikuu kimoja: KUPIGANIA MASLAHI YA WASANII WA HIP-HOP, NA USTAWI WA MUZIKI HUO!

-Kaveli-
 
Kwenye video ya Geez Mabovu napotoka mimi nadhani kuna footage za Okoa Hip hop movement.
 
Kaveli

Asante sana Kaveli umejibu vizuri sana, nimeridhika. Umegusa hata angle ambazo nilikuwa nimezisahau ktk hoja yangu.

Kuhusu ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hizi 'sarbotage' na mimi pia nilikuwa nahisi hao hao ulionitajia kwa kificho (ambao ANTI VIRUS imewachana kwa uwazi zaidi), nimepata uelewa mpana zaidi kwa mchango wako huu kiongozi.

Akina LIKUD karibuni tupate na mchango wenu hapa.

Ant virus ilikuwa hasa ni kuokoa unyonyaji wa clouds

1) Walikuwa wanapigania maslahi ya wasanii wote

2) Walikuwa wanapigania studio ya ngoma records (Tuddy Thomas)

Kuna mixtape kadhaa walitoa nyimbo nyingi Walikuwa wanatukana

hasa kuna moja ilikuwa inaitwa zingu nikuzingue humu kulikuwa na sauti ya mdada yupo njema beat ilikuwa ya Dr Dre
 
Last edited by a moderator:
upo nchi gani bob ?
Leo ndio mazishi iringa

mkuu, point of correction: Jana (Alhamisi 13 November 2014) ndo mazishi yalifanyika katika makaburi ya Mlolo, Iringa.

-Kaveli-
 
Hivi geez mabovu nae amefariki au mtoa thread umechanganya!

Mkuu 'moment of truth'... Geez keshafariki. Mazishi yake yalifanyika jana. That's the 'truth' na sasa ni 'moment of silence'

-Kaveli-
 
Okoa Hip Hop ni harakati maalumu zilizoanzishwa mwishoni wa mwaka 2007 baada ya kilio cha mashabiki wa hip hop kuhusu kudidimia kwa muziki huo pendwa. Project hii ilijumuisha wasanii kama Salu-T, Saigon, Magazijuto, Fid Q, Nako 2 Nako, Geez Mabovu (R.I.P), Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Jay Moe, Adili , Mapacha, Blac, Langa (R.I.P), n.k

ADILI a.k.a HISABATI ndie founder wa platform hii, madhumuni ya idea yake hii ilikuwa ni kupigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama ilivyo katika aina zingine za muziki hapa bongo. Pia ni kuhakikisha kila msanii (washiriki) anapata nafasi ya kupromote kazi zake kupitia platform iyo, maana watu waliohudhuria harakati izo waliweza kujipatia bidhaa za wasanii wa hip hop waliomo katika mradi huo iwe ni tapes, tshirt, cd, n.k

Sababu kuu ya project hiyo ilikuwa ni KUIOKOA hip hop kabla haijapotea kabisa in Tanzania community. Ni kupigana na mnyonyaji mkuu wa muziki huu bongo ili kuiweka HIP HOP kwenye hadhi yake inayostahili kuwepo.

MNYONYAJI mkuu ni MUSIC INDUSTRY nzima, in particular the MEDIA. Mnyonyaji huyu ameshaweka mikakati makini sana kuhakikisha kwamba hip hop haifanyi vizuri kabisa bongo. Katika moja ya Interview za gwiji Adili mwanaHisabati, aliwahi kusema hivi: “Iwapo hatutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunafanya hizi harakati, kweli kabisa hip hop itapotea na kutakuwa hakuna wa kuikoa kwani sisi wanahip hop ndio wa kuiokoa, no one else”

Katika PROJECT hii, mambo mengi yalifanyika, ikiwa ni pamoja na kutoa documentary ambayo inaelezea historia nzima ya Hip hop ya bongo, pia documentary hii ilijumuisha exclusive videos za wasanii washiriki. Documentary hii iliwahi kuoneshwa pia kwenye tamasha la USIKU WA HIP-HOP (HIP HOP NIGHT) pale Dar Live Mbagala, mwezi March 2012.

In short, OKOA HIP HOP ilikuwa ni harakati za kuleta mapinduzi ya kuhakikisha kwamba wasanii wa hip hop wanaungana katika kupigania haki zao na muziki huu. Harakati hizi zilifanyika kwa tour mbali mbali mikoani.

NOW, Back to the concern ya mleta uzi: Je ni nani/akina nani walikuwa nyuma ya hujuma hizi za kuuhujumu (sarbotage) huu muziki hadi wasanii hawa kuamua kuanzisha hatua za makusudi kuuokoa?

RESPONSE: kumbuka vizuri harakati za ANTI-VIRUS and its primary 'target', then jibu la swali lako utalipata. ANTI-VIRUS movements ilikuwa ni muendelezo wa OKOA HIP HOP movements. Thus, harakati za anti-virus project zilikuwa ni 'next episode' ya okoa hip hop project with the same theme, same target, same objectives, same goal, but with different strategies.

Hopefully mchango wangu umekupa mwanga kidogo japo pa kuanzia.

-Kaveli-

Uko vizur mkuu ni sahihi kabisaaaaaa
 
Uko vizur mkuu ni sahihi kabisaaaaaa

ahsante mkuu Mc Luggy, tunajaribu kujifunza zaidi kuhusu harakati za muziki wa Hip Hop (bongo based). Na inabidi kwakweli wadau tuzidi kuitetea hip-hop kwa hali na mali, muziki huu ndo ukombozi wa jamii ya mtu mweusi. Ukombozi kwa maana ya movements (harakati) na knowledge. Katika wimbo 'Hip Hop Lives' by KRS ONE, mnyamwezi huyo anasema hivi: ''HIP is for movements, HOP is for knowledge''.

Dedication: 'Nakupenda Hip-Hop' by Roho 7

-Kaveli-
 
Ant virus ilikuwa hasa ni kuokoa unyonyaji wa clouds

1) Walikuwa wanapigania maslahi ya wasanii wote

2) Walikuwa wanapigania studio ya ngoma records (Tuddy Thomas)

Kuna mixtape kadhaa walitoa nyimbo nyingi Walikuwa wanatukana

hasa kuna moja ilikuwa inaitwa zingu nikuzingue humu kulikuwa na sauti ya mdada yupo njema beat ilikuwa ya Dr Dre

Kuna kipindi Mgosi Mkoli aliwahi kuhojiwa;
Swali: Kwanini katika mixtape zenu mnatumia sana lugha za matusi?
Mkoloni: Hapana sisi hatutumii lugha za matusi, bali tunatumia lugha kali. Na hii ndo lugha ya mitaani. Na tumeitumia hiyo lugha ili kusisitizia mambo tunayoyapigania.
 
Mkoloni wa Wagosi Wa Kaya, emcee asiyemeng'enya maneno, it's all about truth. Huwa nawakubali sana hawa wagosi, hasa yule Dr. Jonh. Kuna pini moja ivi inaitwa 'Uhamiaji' by Dr. John, huwa naipenda sana hii ngoma, kazungumzia kuhusu bureaucracy (urasimu) wa sekta nzima ya uhamiaji (immigration authority) ya bongo, katika kupata Passports za kusafiria. Amepaka sana umo ndani. Lakini masikini media zetu, nyimbo kama hii hutaisikia ata siku moja ikirushwa redioni ama kwenye Tv.

-Kaveli-
 
Aisee rip jamaa duh wakuu kichwa kilitibuka siku mbili hizi!mbele wewe nyuma sisi!
 
How can HiP HoP be dead, if Wu tang is forever!!
 
Attachments

  • 1415969536096.jpg
    1415969536096.jpg
    43.5 KB · Views: 120
Back
Top Bottom