Programu Ninazotumia

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
233
Siku za karibuni nilipata computer nikaamua kuondoa operating system iliyokuwepo na kuweka ya kwangu mwenyewe ambayo haikuwa na programu zozote za ziada kama nyingi zilivyokuwaga .

Baada ya hapo nikafikiria kuhusu programu za kuweka ambazo zitafanya matumizi ya computer yangu yawe bora zaidi , ikitokea tatizo linalohusu software nieweze kujua kwa urahisi na hata hardware wakati mwingine unaweza kujua kutokana na zile programu nitakazo weka .

Kwanza nilianza kuweka Hard Disk Health , programu hii inasaidia kuangalia ( monitor ) matumizi ya harddisk ya computer yangu , inazunguka kwa spidi gani , inatumikaje , joto na vitu vingine kibao tu kwahiyo siku harddrive yangu ikiwa ina tatizo lolote lile hiyo programu itaniambia , kwahiyo ni mpya kwa muda ule sikulazimika sana kuitumia .

Nikaingiza antivirus katika antivirus nilikuwa makini sana kutokana na baadhi ya antivirus nilizowahi kutumia au kutumia kwa watu wengine na nilivyoona matumizi yake mfano Norton 2006 mpaka 2008 huwa ni kubwa licha ya ukubwa wake unavyofanya install inakwenda sehemu nyingi sana kiasi kwamba kitu kama Office ikicorrupt Norton inaweza kuacha kufanya kazi , halafu pia kuna aina za virus ambazo huwa zina disable Norton ukiacha hayo mfano windows iki corrupt kitu kama bootsector unapolazimika kufanya repair kama una Norton unawez akutumia zaidi ya masaa 48 kwa sababu hii antivirus inascan kila file linaloingia katika hiyo computer wakati wa kukopy au kufanya registration inapobakia dakika 13 kumaliza repair wazo la kutumia Norton likaisha .

Nikafikiria kuhusu Symantec Cooperate , hii ni nzuri na Portable lakini kuna wakati usipofanya update mapema huwa inazima computer au kurestart computer hii ina fanana sana na AVG Free Edition na AVG full Version hizo zote ni portable tofauti yake kubwa ni kwamba AVG ina sehemu ya Heal kama umepata virus unaweza kutibu lakini Symantec sio hiyo huwa ina delete au kupeleka katika quarantine , lakini sijui kuhusu version zingine za kisasa za Symantec kama zina heal , cure au clean .

Kukawa kuna Mcafee Version 8.5 hii nayo ni nzuri sana , sema haiwezi kutoa virus ambaye ana haribu mfumo wa kuboot katika Operating system au Autorun katika Flash Disk, kama umewahi kukutana na virus kama broontook huyu huwa anakula file moja linaloitwa Win Ini katika Windows XP basi ukiwa na Mcafee Version hiyo na zingine nyingi huwa ina Delete hilo file utashindwa Kulogin mpaka utumia CD ya windows kufanya Repair sasa shida zote hizo za nini ?

Sema Mcafee ina msaada mkubwa sana katika kuondoa Virus Wanaozaliana kwa wingi wenye ex ya SCR ,hawa scr huwa wanashambulia folders zaidi haswa katika vifaa vya kuchomeka kama Flash Disk au kitu chochote external kwahiyo ukila mwereka ukiwa na virus huyo katika hizo flash halafu una mcafee basi yenyewe huwa ina delete hizo folder zote bila kuuliza , ukitumia AVG inasema hakuna virus , Ukitumia Symantec itasema kuna virus lakini inapeleka katika Quarentine , ukitumia Kaspersky haitafanya chochote na haita delete chochote .

Pia huwa inashambuliwa na virus mmoja Anayeleta file la AVP katika start up , kila unapowasha computer yako utaona vitangazo vya AVP mpaka utafute utilitly yake inayoitwa ComboFIx au uende katika start up kutumia msconfig udisable hiyo avp kutokutokea tena wakati mwingine ni hiyo Autorun.inf hii mara nyingi ni kama umechomeka flash kaspesky inaweza kutoa hiyo autorun mcafee haiwezi hiyo msg itaendelea kujirudia kila secunde 10 mpaka utoe mcafee au uende katika on access scan udisable message alerts .

Ukitumia Bitdefender inasema kuna virus inapeleka file hizo katika quarentine , lakini inategemea unatumia version gani , kama ni free edition huwa inasema hiyo lakini ukitumia Bit Defender Internet Security 2008 , yenyewe itablock kwa sababu inayo file wall nzuri kabisa inafanya yote haya kama uki update antivirus hiyo punde tu unapomaliz akufanya installation .

Siwezi kukuambia niliamua kutumia antivirus gani , nitaonekana natangaza biashara za watu wengine wakati sio nia yangu ni shauri ya mtu mwenyewe kutumia antivirus anayotaka yeye mwenyewe ilimradi anaweza kufanya kazi zake bila matatizo yoyote yake .

Katika matumizi ya computer kwa kawaida kuna programu za kutumia katika kufanya haya na yale mfano computer iko slow , tatizo likawa sio RAM , sio Virus , sio hiyo unavyofikiria wewe ufanye nini utatumia nini tena kuhakikisha unaweza kuirudisha computer yako katika hali ya kawaida ?

Virus wengi siku hizi na Antispyware wengi wana haribu mfumo wa System Restore mfano katika Windows Xp kwahiyo hatutegemei sana hiyo kama ukipata matatizo ya aina hiyo je ufanyeje ?

MAKALA HII ITAENDELEA SIKU INGINE

AHSANTE KWA KUSOMA
 
Back
Top Bottom