Wakuu awali napenda tumkumbuke kwenye maombi yetu msanii Joseph Haule alejee kwenye majukumu yake ya kila siku.
Pia Jana tulikuwa twazungumza juu ya jay na ubishi ukaja nani mkali kati ya jay na Sugu. Eti yupi mkali?
Sugu mashairi yake yanauhalisia sana. Ukimsikiliza unaona kabisa anaimba mambo ambayo yapo kihalisi mtaani, au yamemtokea. Anaweza akawa hana vina vya kupamba kama JAY lakini ana uhalisia sana. Namkubali sana kwa hilo.