Profesa Peter Msolla (mbunge) umechemsha

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Kwa ProfesaPeter Msolla salam.

Nikiwa mjiniTel.Aviv nilisiki jana Profesa anasema bungeni eti wapinzani kutawala nchi hii wasahau labda wakatawale sayari nyingine.

Nadiriki kumwambia kwamba ni profesa kweli kwa maana amefundisha chuo kikuu lakini kwa hili kadhihirisha kwamba ni mpumbafu kwa sababu zifuatazo:-

1. Kuna mambo mengine hutokea verydramatic kiasi huwezi kuyazania kama yatatokea, wala huwezi kuyapigia mahesabukama profesa ulivyofanya, mfano

2. Kufungwakwa bank ya meridian Biao wateja walikuta tu milango imefungwa without any notice,wateja hao ungewauliza jana yake kwamba bank itafungwa wote wangekukatalia kabisa kama Profesa anavyozani eti wapinzani hawawezi tawala nchi hii

3. Kimbunga cha SUNAMI kilivyoikumba pwani ya Indonesia watu wala hawakupigia mahesabu jambo hili lilitokea gafla mno, mambo mengine kutokea gafla mno huwezi kupiga hesabu.

4. Mzee Kaunda aliambiwa akafanye kampeni ili UNIP iendelee kutesa madarakani alijibu hamana haja ya kampeni UNIP itashinda tu yeye akaenda kucheza gofu, baadae kilichotokea hata Profesa Msolla anakifahamu.

5. Utawala mkongwe wa makaburu ulianguka zama hizo hata mimi nilikuwa nawazo ya kama Profesa Msolla kwamba wapigania uhuru wasingeweza kuwatoa makaburu madarakani nilidiriki kumwambia mpigania uhuru mmoja kwamba wao kujitawala labda ipitemiaka 50, alicheka sana akanijibu how far are you sure, ilipita miaka 5 tangu nimkejeli Afrika ya kusini ikajikomboa.

6. Hata mdogo wake Peter Msolla, Dr. Hamza Msolla aliamini yeye atafia akiwa meneja utawala AMREF Tanzania lakini asubuhi moja tu alikuta barua mezani kazi hamna hakuamini macho yake na sasa yuko Tabata anasaga lami.

7. Kwanye haya mambo ya kijamii Profesa usijaribu kuwasemea wengine ukafikri na wao wana mawazo kama ya kwako, profesa unajidanganyasana kwani kura hupigi peke yako kwa hiyo huwezi jua wenzake wanawazanini. Nijitolee mfano mimi mwenyewe niliwahi kuwasemea wanawake kwamba siyo ubinadamu kujamiiyana wakati wa hedhi.(mimi ebaeban ni mwanaume),walionipinga ni wanawake wenyewe, wakanijibu wewe kwenda zako kama mwezako alikuwa safari na amerudi amekukuta uko mwezini unampatu unataka achepuke?

Basi nikaadhirika kama Profesa utavyoadhirika.

Kujiamini sana ndiko kulikomponza Yuda Eskariote akaitwa msaliti hadi leo, kumbe yeye alikuwa na nia nzuri tu,aliamini kwamba hamuna atayeweza kumkamata Yesu maana waliisha jaribu watu mala nyingi wakashindwa na yeye ikishuhudia,kitu ambacho hakujua ni kwamba ilibidi mtu afe ili neno litimie, hivyo kuona yesu amakamatwa alichanganyikiwa ndio maana akataka awarudishie vile vipande vya dinali, kama alivyojiamini yuda naProfesa Msolla anajiamini hivyo hivyo.

Mwisho Professa Msolla, No situationis permanent, kama huamini mwulize Omaru Dikko wa Nigeria enzi za utawala wa Shehu Shagari uzuri Diko yuko hai professa wasiliana nae umwambie maneno yakohayo usikie majibu.
 
Huyo Prof
anapima upepo !unaumiza kichwa kumpa store ndefu
anahofia u Prof wakati UKAWA wamechukua nchi.
 
Tungesema wabunge wapewe tuzo ya elimu kutokana na uwasilishaji wa hoja bila shaka MNYIKA, LISSU, FILIKUNJOMBE wangetunikiwa uprofesa na hawa maprofesa wangetunikiwa cheti yaani certifiacate
 
Haya ndiyo matokeo ya wanataaluma kuacha kazi zao walizobobea na kudandia siasa, tena siasa uchwara za kuchumia tumbo kama hizi za kwetu. Ili wafanane na wenzao wanataluuma wanapoingia katika siasa, hasa kupitia chama tawala, usitarajie kuwa ataumia usomi wake kwa manufaa ya nchi. Kwani, akina Prof. Msolla, Magembe, Dkt Migiro si wamekwenda huko bungeni kwa maslahi yao binafsi? Kwa hakika wangekuwa na uzalendo na mapenzi kwa nchi hii wangebaki vyuoni kufundisha vijana wetu. Wameingia siasa kufukuzia maslahi binafsi!
 
Hilo jamaa Fataki per se. Ni aibu hata kumwita Professor. Akiwa SUA alikuwa anafanya ufataki kwa mabinti wa Lecturers wenzie. He better keep quite.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom