Kwako Prof. Peter Msolla, Mbunge

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Kwa Profesa Peter Msolla salam.

Nikiwa mjini Tel.Aviv nilisiki jana Profesa anaropoka bungeni eti wapinzani kutawala inchi hii wasahau labda wakatawale sayari ingine.

Nadiriki kumwambia kwamba ni profesa kweli kwa maana amefundisha chuo kikuu lakini kwa hili kadhihirisha kwamba ni mpumbafu kwa sababu zifuatazo:- 1.

Kuna mambo mengine hutokea very dramatic kiasi huwezi kuyazania kama yatatokea, wala huwezi kuyapigia mahesabu kama profesa alivyofanya, mfano

i. Kufungwa kwa bank ya meridian Biao wateja walikuta tu milango imefungwa without any notice,wateja hao ungewauliza jana yake kwamba bank itafungwa wote wangekukatalia kabisa kama Profesa anavyozani eti wapinzani hawawezi tawala inchi hii

ii. Kimbunga cha SUNAMI kilivyoikumba pwani ya Indonesia watu wala hawakupigia mahesabu jambo hili lilitokea gafla mno, mambo mengine kutokea gafla mno huwezi kupiga hesabu.

iii. Mzee Kaunda aliambiwa akafanye kampeni ili UNIP iendelee kutesa madarakani alijibu hamana haja ya kampeni UNIP itashinda tu mimi naenda kucheza gofu, baadae kilichotokea hata Profesa Msolla anakifahamu.

iv. Utawala mkongwe wa makaburu ilianguka zama hizo hata mimi nilikuwa nawazo ya kama Profesa Msolla kwamba wapigania uhuru wasingeweza kuwatoa makaburu madarakani nilidiriki kumwambia mpigania uhuru mmoja kwamba wao kujitawala labda ipite miaka 50, alicheka sana akanijibu how far are you sure, ilipita miaka 5 tangu nimkejeli Afrika ya kusini ikajikomboa.

v. Hata mdogo wake Peter Msolla, Dr. Hamza Msolla aliamini yeye atafia akiwa meneja utawala AMREF Tanzania lakini asubuhi moja tu alikuta barua kazi hamna hakuamini macho yake na sasa yuko Tabata anasaga lami.

2. Kwanye haya mambo ya kijamii Profesa usijaribu kuwasemea wengine ukafikri na wao wana mawazo kama ya kwako, profesa unajidanganya sana kwani kura hupigi peke yako kwa hiyo huwezi jua wenzako wanawaza nini.

Nijitolee mfano mimi mwenyewe niliwahi kuwasemea wanawake kwamba siyo ubinadamu kujamiiyana wakati wa hedhi. (mimi ebaeban ni mwanaume),walionipinga ni wanawake wenyewe, wakanijibu wewe kwenda zako kama mwezako alikuwa safari na amerudi amekukuta uko mwezini unampa tu unataka achepuka? Basi nikaadhirika kama Profesa atavyoadhirika.

3. Kujiamini sana ndiko kulikomponza Yuda Eskariote akaitwa msaliti hadi leo, kumbe yeye alikuwa na nia nzuri tu, aliamini kwamba hamana atayeweza kumkamata Yesu maana waliisha jaribu watu mala nyingi wakashindwa na yeye ikishuhudia,kitu ambacho hakujua ni kwamba ilibidi mtu afe ili neon litimie, hivyo kuona yesu amakamatwa alichanganyikiwa ndio maana akataka awarudishie vile vipande vya fedha, kama alivyojiamini yuda na Profesa Msolla anajiamini hivyo hivyo.

4. Mwisho Professa Msolla, NO SITUATION IS PERMANENT, kama huamini mwulize Omaru Dikko wa Nigeria enzi za utawala wa Shehu Shagari uzuri Diko yuko hai professa wasiliana nae umwambie maneno yako hayo usikie majibu.
 
Salaam zako nzuri sana, lakini pamoja na mifano yako mizuri upinzani uliopo bado ni mdogo na hauna msisimko kabisa. Wapo wazuri wanaojenga hoja za maana lakini hawasikiki/ hawaonekani kuyafanya yale wanayoyasema. Kama ulivyo mnukuu Prof. Siyo rahisi kwa upinzani kushika dola kwa miaka ya karibuni labda wananchi wakubali kuondokana/kukataa umasikini uliokidhiri. Hamasisha watu wakajiandikishe kwa ajili ya kupiga kura na wapige kura siku ikifika hapo ndipo kitakuwa kipimo tosha cha upinzani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom