Profesa Lipumba: Rais Magufuli chondechonde njaa kali

Profesa Lipumba: Rais Magufuli chondechonde njaa kali

yeye si anapigiwa saluti? kelele za nini sasa.au anataka apigiwe mizinga 21?
mwe!
 
Samahani, naombeni mnisaidie. Lipumba si alitangaza kuacha siasa August 6th, 2015? au ameshatangaza tena kurudi?. Na hivi amejiunga na UKAWA?. Na huko UKAWA Lowasa ameshaondoka au bado yupo?. Nakumbuka aliondoka sababu ya Lowasa.

Naombeni msinitukane mie.
amerudia siasa alizojifunzia Rwanda. ameachana na CUF-UKAWA ana chama chake cha CUF-CCM!
 
Siku walipoondoka Dr Slaa na Prof. Lipumba upinzani umepwaya kwa sababu hoja ya msingi ya ufisadi iliyoipa nguvu upinzani wameipokea upinzani kwa sababu ya kuziba masikio na kutokuwa na msimamo huku wakitumia nguvu kujaribu kuisafisha.Hao walikuwa na spirit ya upinzani (sina uhakika na spirit aliyonayo Profesa kwa sasa) Kwa sasa hoja hiyo kila upande wanaitumia (wanashare).Hakuna msafi ndio maana JP anaburuza anavyotaka.
Infact kinara wa kambi ya upinzani Lowasa anatumia soft kinder or more gentle type of politics ambayo haina madhara makubwa kwa chama tawala na anaonekana bado ana mapenzi makubwa na CCM ila mazingira yalimfanya aondoke.
Practically Lowasa alikuwa mtaji mkubwa kwa kipindi cha uchaguzi kwa upinzani but honestly kwa political neutral/soft political strategy yake hawezi kuwa msaada tena.
Pengine mtaji pekee wa upinzani uliowadondokea kwa bahati ni JP mwenyewe na matendo yake.
 
Process njaa asejua baya wala zuri
 
Hayo ni maneno ya mchumi aliyeboboa ambaye aliwahi kuwa mshauri wa uchumi wa Mzee Ruksa?
Hana jipya hata moja la kutuambia. Msukuma na Mnyamwezi wote sawa ni wale wale tu. Very primitive
 
Ile Slogan ya 1995 naikumbuka Mkimchagua Mrema Mtalemaa,Mkimchagua Mkapa mtatoka kapa,Mkimchagua Lupumba mtakuwa wapumbavu na Mkimchagua Cheyo Mtapata Mapesa...
 
KILIO cha hali ngumu ya maisha tangu kuanza kwa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, kimemgusa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba ametoa wito maalumu kwa Rais John Magufuli kusikiliza kilio hicho cha wananchi kwa kulegeza kamba ya kubana matumizi na kuwaandalia wananchi mazingira mazuri ya kumudu maisha yao.

Profesa Lipumba alitoa wito huo juzi katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Kijichi iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam kupitia chama hicho, Khalid Shamas.

Lipumba ambaye ni profesa aliyebobea katika taaluma ya uchumi, alisema sera ya kubana matumizi haina ubaya, lakini jambo hilo, lazima liendane na mpango wa kuwasaidia wananchi katika kujipatia riziki zao.

“Watu wanapigika na wengine wanalazimika kufunga bila kunuia, halafu tunajigamba tumefanikiwa kukusanya fedha nyingi kwa kubana matumizi. Hiyo inatusaidia nini wapiga kura wako, mheshimiwa rais?” alihoji Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba ambaye aliwahi kuwa mshauri wa mambo ya uchumi katika Serikali ya Awamu ya Pili na mtaalamu aliyewahi kutumiwa na mataifa mengi, ikiwamo Uganda kushauri masuala ya uchumi, alisema uchumi unaokua bila kuonekana mifukoni mwa watu hauna tija.

“Hizo sera (za kubana matumizi) zinaweza kuwa nzuri sana, lakini umesahaulika mpango wa kuona ni kwa namna gani wananchi wanasaidiwa kumudu maisha yao. Leo vijana wanapigika na hakuna msaada.”

Profesa Lipumba aliishauri Serikali kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri ili waweze kuboresha maisha yao na kujenga mazingira ya kutafsiri ukuaji huo wa uchumi katika maisha ya wananachi wa kawaida.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Profesa Lipumba imekuja ikiwa tayari Rais Magufuli ameeleza kuwa mpango huo wa kukata mirija ya upatikanaji fedha kiholela, umelenga kuwafanya watu wafanye kazi.

Rais Magufuli ambaye Serikali yake inaongozwa kwa kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’ alisema anataka kila Mtanzania ale kwa kipato chake halali. Akaamua kusitisha vikao na semina za taasisi za Serikali mahotelini na kupunguza safari za nje za mawaziri, huku akiboresha ukusanyaji kodi kama moja ya hatua ya kutaka taifa lijitegemee.

Amnadi mgombea wake

Profesa Lipumba aliwaomba wakazi wa Kijichi kumchagua Khalid Shamas kuwa diwani wa kata hiyo katika uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Januari 22, ili apeleke kilio cha ugumu wa maisha katika vikao vya halmashauri.

“Siyo rahisi CCM kusema ukweli kuhusu jambo hilo. Hapa tunahitaji mtu mwenye misimamo tofauti kidogo. Mchagueni Shamas akawakumbushe CCM kwamba pamoja na mipango yake, watu wanapigika… Hakiii...”

Akizungumza katika mkutano huo, Shamas aliomba achaguliwe akieleza kuwa amekuja na mipango mbadala ya kuwaletea wakazi wa Kijichi maendeleo endelevu.

“Wagombea wote hakuna aliyefika hapa na kablasha la kazi. Mimi ninalo, hili hapa,” alisema Shamas akionyesha karatasi aliyoishika mkononi.

Aliendelea “Humo kuna mambo mengi. Mkinichagua nitaanza na elimu. Nitahakikisha nasimamia sera ya CCM ya elimu bure itoe elimu bora na siyo bora elimu. Nitasimamia ujenzi wa maabara katika shule zote za Sekondari, ujenga soko katika kila mtaa, mabweni kwa wanafunzi wa kike na umeme mashuleni.

Uchaguzi mdogo wa Kijichi unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kupitia CCM, marehemu Underson Charles.

Chanzo: Jambo leo


======

Kilio cha hali ngumu ya maisha tangu kuanza kwa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, kimemgusa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Ibrahim Lipumba ametoa wito maalum kwa Rais John Magufuli kusikiliza kilio hicho kwa wananchi kwa kulegeza kamba ya kubana matumizi na kuwaandalia wananchi mazingira mazuri ya kumudu maisha yao

Profesa Lipumba alitoa wito huo juzi katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi iliyoko Temeke jijini Dar es salaam kupitia chama hicho, Khalid Shamas.
Hata wewe Brutus? (Brutus alivyomsaliti Julius Caesar- Shakespeare)
 
Naona Kaenda kumwambia mkulu hali ni ngumu, mkulu hajankawiza kamwambia ajiongeze. Mbona tayari saa hii ruzuku ya Cuf imeota mbawa?
 
Si naskia kaiba hela za ruzuku CUF milioni 300 jana? Wamegawana zikaisha?
 
Naona Kaenda kumwambia mkulu hali ni ngumu, mkulu hajankawiza kamwambia ajiongeze. Mbona tayari saa hii ruzuku ya Cuf imeota mbawa?
kajiongeza kweli kweli kavunja sheria zote mmaee
 
Mkuu amemskia na tayari kinyume cha sheria amepewa pesa za ruzuku za cuf.
Ikumbukwe huyu lipumba alijitoa wakati wa uchaguzi na kampeni. Na ruzuku ni matokeo ya jitihada za vyama katika uchaguzi. Chama kikifanya vizuri ruzuku kubwa.
Cuf ilifanya vizuri bila ya lipumba. Na saa Magu anakuja kuchukua fedha za umma kumkabidhi mhuni aliemtuma kufanya fujo na kuikoroga cuf.
Hakika hili alofanya magu ni kosa kubwa sana . Anatumia madaraka yake vibaya na fedha za umma kuua democrasia kwa kuwapa pesa maharamia hawa pesa za kulisha majambazi.
Hii ni moja katika legacy atayo tuachia magu..ufusadi dhidi ya democrasia...
Hili la kumpa lipumba ruzuku sio la hazina au msajili....ni magu tu...watu wanakufa njaa lakini anahiari kutoa hela kinyume cha sheria ili kujifurahisha kuwa sitakua na mpinzani 2020.
Ukweli wanamdanganya
 
Juzi wakati napitia baadhi ya magazeti ya Tanzania, Luna gazeti lilimkariri Mh.Prof.Lipumba Mwenyekiti aliyejiuzulu Na kurudi wa CUF akimwambia Mh.Rais Magufuli kuwa nchi ina njaa.Sina uhakika kama Prof.Lipumba anazungumzia njaa Kwa dhati kwani Chama cha CUF kimekuwa kinapokea Ruzuku ya Mil.400 ambazo in kodi za hao masikini wanyonge wa Tanzania.Niliamini Prof.Lipumba angeiambia Serikali hiyo Ruzuku ipelekwe kwenye maeneo yenye njaa Kali ambako hata chama chake CUF kina
wafuasi.
 
Back
Top Bottom