Profesa Lipumba chonde chonde, ulijiondoa CUF kwa hiari yako mwenyewe

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
994
1,567
Profesa Lipumba uyafanyayo Mungu anakuona. Ulijiondoa ndani ya CUF 'kwa hiari yako mwenyewe', tena katika kipindi kigumu sana kwa chama, ambapo kilikuwa kikikuhitaji sana.

Ulijiondoa kwa kujiamini na kiburi kingi. Jambo la kushagaza ukalazimisha kurejea ndani ya chama wakati chama kilishajipanga chenyewe kuendelea bila wewe.... hakikuhitaji kabisa.

Katibu Mkuu na wenzake wamehangaika na kuwekeza sana kwenye chama hiki kwa maslahi ya wengi wa bara na visiwani. Haya unayoyafanya hivi sasa yanadhoofisha nguvu ya chama na maslahi ya chama, wafuasi na wapenda demokrasia ndani na nje ya Tanzania.

Imeripotiwa kwamba umetengua uteuzi wa wakurugenzi sita wa chama, eti kwa kosa la kutohudhuria kikao cha kamati ya utendaji!!?? Kwa faida ya nani?

Haya unayoyafanya wewe unayafanya kwa maslahi ya nani? Unawaumiza watu wengi sana ndani na nje ya chama, na anayeumiza wengi Mungu anamuangalia! Unawacheza shere wenzako waliokijenga chama kwa miaka mingi tena katika mazingira magumu.

Unachofanya ni kukibomoa chama, ili iweje, upate nini!?? Hata kama kuna maslahi binafsi unapata (Labda), lakini hayalingani kabisa na maslahi mapana ya uwepo wa chama.

Inatambulika sana, na itaandikwa kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kwamba, amepata kutokea mtaalamu nguli wa uchumi ambaye ni wewe. Nadhani nchi yetu, wewe mwenyewe na familia yako itaona fahari kwa hilo.

Bora ibaki hivyo hivyo, isije kutokea ukaandikwa kwenye vitabu vya historia kwamba umefanikisha kwa kiwango kikubwa kuua chama hiki, ungelipenda hilo? Tuombe lisitokee.

Mungu anakuona na wapenda demokrasia pia wanakuona. Chonde chonde, hebu ona soni hata kidogo basi! Kwa maslahi ya wengi, hebu rudi hatua moja nyuma uwafikirie na wengine badala ya kujifikiria wewe tu.

Maana Mungu anakuona!
 
images
images
 
Back
Top Bottom