Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,744
Mwanaharakati huru Cyprian Musiba amedai kuwa viongozi wengi wa vyama vya upinzani nchini si wa kweli na wanatumia nafasi zao kama chanzo cha kipato badala ya kutetea maslahi ya wananchi.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Jambo TV, Musiba amesema vyama vya upinzani vimegeuka kuwa ajira kwa baadhi ya viongozi wake, huku akidai kuwa baadhi yao wanajihusisha moja kwa moja na chama tawala, CCM, kwa lengo la kujinufaisha kifedha.
Aidha, ameeleza kuwa viongozi wa upinzani maarufu kama Profesa Ibrahim Lipumba, John Cheyo, Zitto Kabwe, Seif Sharif Hamad (marehemu), na Freeman Mbowe hawajawa na athari kubwa kwa maisha ya wananchi, akisisitiza kuwa wengi wao wapo kwa maslahi binafsi na ya familia zao.