Prof shirvji na dhana ya ubinadamu, haki za binadamu na utawala bora

Omulangi

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
1,036
265
Katika hafla ya kumtunuku Dr Slaa tuzo ya maji maji inayotolewa kila miaka 5 na Kituo cha sheria na haki za binadamu Dr Shirvi ametoa mada kuhusu haki za binadamu na utawala bora iliyokoga nyoyo za watu. Kituo hiki kiliandaa tafrija maalum kuanzia saa 1 jioni alitinga akiwa ndani ya suti nyeusi, pamoja na mama Slaa akiwa ndani ya blausi ya black na sketi viatu vya blue na mkoba wa blue na make up iliyomfanya aonekane mweupe pee. Kabla ya mambo mengi Dr Shirvji akamwaga material yake hapo. Binadamu sio suala la kibiolojia alianza. Binadamu ni dhana ya kiitikadi, kijamii na kifalsafa. Kuna wakati katika miaka ya katika 1500 hadi 1900 mwafrika hakutambuliwa kama mwanadamu. Mwafrika alikuwa ni bidhaa na bidhaa haina haki yoyote. Chunguzeni katika rekodi hata za mahakama zipo kesi zilizoamualiwa na majaji wakikana utu wa mwafrika. Wakisema huyu si binadamu vinginevyo asingeweza kuuzwa na kununuliwa.Hapa msisitizo wa magharibi ulikuwa ni kukuzanya mtaji. Ndiyo maana unapozungumza juu ya binadamu lazima uangalie ni itikadi ipo iliyopo.

Unaposema haki pia lazima ujue kuwa haki haiwezi kuwepo kwa mwanadamu aliyechumwa kama tunda toka mtini na sasa unajadili tunda kama vile linatokea hewani. Lazima uanagalie jamii anakotoka huyu mwanadamu. Hawezi kupata haki nje ya jamii yake. Kuna wakati hatukujua kama wanawake ni binadamu hiyo awamu ni kama inaelekea kupita. Sasa tunajadili ikiwa watoto ni wanadamu au la. Wanazo haki zozote au la.
Wakati mwingine tumewaambia watu waliotujia wakitaka msaada wa sheria kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Inategemea unaposema haki unazungumza kwa mtizamo upi kulingana na itikadi yako. Haki unayoijua katika jamii yawezekana sio haki inayotajwa na sheria. Inategemea sheria zile zimeandaliwa katika itikadi ya namna gani. Kama ni katika itikidadi ya kibwenyenye inayosisitiza bidhaa (commoditization) na privatization ambapo hata milima kama ule wa Oldonyo lengai (unaoabudiwa na Wamasai) unabinafsishwa si ajabu siku moja tutaambiwa Kirimanjaro pia umebinfasishwa. Ikiwa misitu, mabonde na maji vinabinafsishwa bado kidogo na hewa itabinafsishwa ili iwepo kampuni ya kuuza oxygen. Usidhani sheria katika mazingira hayo zitatoa haki kwa mtizamo wa mtu asiyekuwa na uwezo wa kiuchumi.

Dhana ya utawala bora mimi naikataa kabisa kabisa. Nani anayetoa cheti cha mtawala bora? Si ndio hao hao wanaotoka mrahisishe kutoa vibali vya uwekezaji ili katika masaa 24 wawe wamepata leseni zote. Hapo wanasema wewe ni mtawala bora. Mtawala yeye anatawala watu kwa malengo na manufaa yake. Sisi tulikuwa na dhana ya kiongozi bora. Si mtawala. Katika azimio la Arusha hakuna mahali popote tulizungumza habari za watawala bora. Kiongozi bora anashirikiana na wananchi, anasimama nao, anawaongoza ili kujitawala wenyewe kwa maendeleo yao. Leo tuna watawala bora wanaotawala kwa maslahi ya wakubwa.

Baada ya Dr Shirvji kukoga nyoyo ndipo ikaelezwa historia ya tuzo ya majimaji. Ni mara ya 2 kituo kutoa tuzo hiyo. Miaka 5 iliyopita ilitolewa kwa jaji Mwalusanya. Yeye alishinda kutokea mhilimili wa dola wa mahakama, kama jaji bora katika kutetea haki za binadamu. Safari hii ni zamu ya mhimili wa bunge ambapo kwa miaka 5 iliyopita Dr Slaa ameshinda tuzo hiyo. Maoni yamekusanywa vijijini, katika mtandao wa face book, katika mashirika na kutoka rekodi za bunge. Dr Slaa aliongoza kwa michango ya kutetea haki za binadamu kwa uzito na wingi wake. Zilitajwa hoja zake binafsi katika EPA, MEREMETA, BENKI KUU, NA RICHMOND. Pia utetezi wake kwa wananchi wa jamii za wafugaji, kufukuzwa kwa watu katika ardhi zao n.k Tuzo hiyo imeenda pamoja na 5 mil Tsh na alikabidhiwa cheque ambayo ni michango toka kwa wafanyakazi wa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa miaka 5 iliyopita.

Ndipo Dr Slaa naye alipata nafasi ya kushukuru akisisitiza hiyo tuzo walitakiwa kupata wengi maana walioibua hizo hoja na kumpa nyaraka ni watanzani wapenda nchi yao. Alisema watanzania wengi wanaipenda nchi yao tena ni wazalendo ila kuna waroho wachache. Akasema tuzo hiyo anaipata ila yeye alikuwa tu mouth piece ya wengi wasiofurahishwa na ufisadi ndani ya nchi. Amewaomba wasikate tamaa waendelee na mapambano ya kuikomboa nchi yao.

In short mambo yamefana!!!
 
Hii nzuri Omulangi... Twataka Tanzania yenye vichwa vya hoja Kama hivi na c majungu na udaku
 
Nimeshangaa mbona vyombo vya habari hakuandika zaidi kuhusiana na hii tuzo ya maji maji na jinsi Dr wa ukweli alivyoipata. Kuna hofu fulani katika jamii imeanza kujengeka kuh kujitambulisha na Dr Slaa?? Nasikia katika vikao vya tathmini vya ccm imeagizwa wote waliokuwa pamoja na mtu huyu washughulikiwe. Inaweza kuwa kweli??? :embarrassed::behindsofa::behindsofa:
 
Back
Top Bottom