Prof. Mwandosya kugombea Urais 2015

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Prof. Mark Mwandosya mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki na Waziri asiyekuwa na wizara maalum amesema kuwa hatogombea tena ubunge bali urais. Ni mwendelezo wa wimbi la watangaza nia linaloshika kasi.

======================================

Chanzo: Mtanzania
 
Listi ya watangaza nia inaendelea. Huyu prof tatizo afya yake. Naye si yuko serikalini kwa muda mrefu, anayo nafasi ya kufanyia kazi mawazo yake kuboresha/kuleta hali nzuri ya maisha. Hana jipya.
Bado Dr Kigwa, Membe,Lowasa,Wasira, Mwigulu, Rits,Migiro,Sita, Nagu,....
 
Wajitokeze hata mia, watz watawapima kwa record zao na kuwachuja
 
Kupunguza hii long list wangeweka kigezo cha kupima ukimwi hawa wagombea ..nina imani tutapata watu wachache sana

Iwe mandatory kwa wale wote wanaotaka kugombea kiti cha URAIS wapimwe afya zao; hilo hufanyika nchi nyingi na hufanywa na jopo la madaktari wenye maadili ya kizalendo. Hili in fact linatakiwa liingizwe kwenye katiba ya nchi kuhusu afya za wagombea wa nafasi za uongozi wa nchi. CCM kwavile viongozi wao wengi ni wagonjwa watalipinga hili kufa na kupona lakini hawatakuwa wanaitendea haki nchi!!
 
Wajitokeze hata mia, watz watawapima kwa record zao na kuwachuja

Watapimwa na CCM yao. Yeye kadai eti Urais ni kazi ya heshima, yaani hajui kwamba TZ Rais ni mtendaji mkuu wa serikali!
 
Nikisikia jina la Mwandosya, naiwazia TTCL hapa ilipo
 
Hatuchagui rais mgonjwa
Wagombea wote wa Uraisi kabla ya mchujo wowote wa kichama kila moja apimwe afya na kuwa na cheti cha uthibitisho kuhusu hali ya afya yake k.m. ukimwi, kisukari,kiwango cha ukichaa,usahaulifu, magonjwa ya moyo, n.k. Sii vyema kuwa na Raisi ambaye muda mwingi anautumia kwa matibabu. Tupate Raisi mwenye afya njema na kama ataanza kuugua akiwa tayari amechaguliwa hilo ni shauri jingine, tutamvumilia aendelee. Lakini kuchagua Raisi ambae tayaari ana mgogoro wa afya ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
 
mkakati maalum wa mafisadi ya ccm kututoa kwenye mambo ya msingi,.rudisheni mabilioni ya escrow,jadilini rasimu ya warioba.
 
nape hapo kiroho kwatu maana prof mark akishinda urais itakuwa zamu yake kutanua kama rizione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…