Mkuu, tatizo la TANESCO linaweza lisiwe Waziri (pamoja na kwamba yeye ndiye mwanasiasa anayewajibika). Waziri anatakiwa awaangalie sana hawa Mameneja wa mikoa. Hivi kazi yao ni nini? hivi wanapangiwa malengo ya kazi na kupimwa utendaji wao wa kazi? Huduma za TANESCO kila mahali ziko chini sana. Sijawahi kuona shirika lenye urasimu mkubwa katika kila huduma kama TANESCO kwa sasa. Lazima Waziri awaburuze hawa Mameneja wa mikoa ili nao wasimamie uwajibikaji wa watumishi wa chini yao.
Tafadhali mkuu kama kuna muhudumu kwa wateja ambaye hajakujibu vizuri au kakufokea naomba utaje jina lake na ni kituo kipi cha emergency ambacho umepiga simu, na pia kama kuna malalamiko zaidi kuhusu ilala kuhusu huduma mbaya au kutosikilizwa kwa namba uliyoitaja basi tafadhali piga 0653062220 ili tuweze kukuhudumia
Mkuu kama unafanya kazi hapo nataka kujua je tatizo lala ILALA mnalitatua liniiiiiiiii hawezekani muhudumu unammuuliza lini anasema wanaendele kutafuta tatizo wiki nzimaaaaaaaaaaaa
when are we going to get stable power ?
HUDUMA ILALA ni MBAYAAAAAAAAAAAAAAA
Mkuu labda useme ni maeneo gani ambayo hayana umeme kwa wiki nzima? Kumekuwa na interuptions kadhaa kutokana na matengenezo ya kiufundi ambayo tumewapa taarifa ila hakuna sehemu ambayo imefululiza wiki nzima! Na pia huduma mbaya kwa upande labda ili niweze kukusaidia zaidi
Mkuu sijasema hakuna umeme ni hiyo interruption more than ten + per day haikubaliki mnatuharibia vitu na jana mlikata kuanzi 19hrs mpa 1 hrs na hii interruption since saturday till yesterday na tatiozo hamlijua lipo wapi as per your support team
Upande ni ILALA shrif Shamba, Bungoni pia
Jamani hebu sometimes muwe mnaiongelea vizuri tanesco kukitokea tatiZo kidogo tuu jipu ina maana hata kwako au cjui kwenu kukitoka tatiZo ni jipu jaribu kutumia msemo wa jipu vizuri kabla hujapublish public kama huyo mmoja alikujibu vibaya nenda kwa meneja wake nakumbuka Tanesco waliwahi kutoa namba za meneja wao Tanzania nzima katika mitandao.tuweni na utu japo kidogo.
Jana ilikuwa ni emergence na tumeomba radhi leo asubuhi kupitia Clouds FM na Upendo Radio njia ya umeme mkubwa ilikatika pale karume hivyo maeneo yote uliyoyataja ni kweli hayakuwa na umeme mpaka saa saba! So matukio kama hayo ambayo hayajapangwa ni vigumu kutoa taarifa mapema ndio maana tunaomba radhi baada ya matengenezo kukamilika. Tunaendelea na maboresho na usisite kutoa taarifa mara tu unapopata matatizo ya kukosa umeme na tutakueleza sababu na kutatua kwa wakati
Hata mimi nashukuru kwamba kuna wasemaji wa Tanesco wanafuatilia majadiliano kwenye mitandao. Kama Msemaji wa Mbeya yupo, tumpe data pia. Maana huu ni mmoja ya mikoa ambayo huduma za Tanesco ziko chini sana! Hata kulipia bills za umeme tu, watu wanashinda kwenye foleni. Ikumbukwe mkoa wa Mbeya ni wateja wachache sana wanaotumia mashine za luku. Emergency section ndio usiseme kabisa! nitampa mpaka reference numbers ya kesi ambazo zimesharipotiwa zaidi ya miezi miwili ambazo hazijashughulikiwa. Kwa sababu wanasema " Hapa Kazi Tu" na sisi hatutanyamaza.