Prof. Muhongo azidi kung'ara

kidesheni

Senior Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
178
Reaction score
35
Umeme wamng'arisha Muhongo

Aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameendelea kupanda chati ya kiutendaji baada ya wanavijiji kupongeza huduma ya umeme vijijini.

Wanavijiji wameripotiwa kukiri kutokutegemea kama siku moja wangaliunganishiwa umeme kwa bei nafuu ya shilingi 27000 sawa na ya kununua jogoo wawili.

Awali walitakiwa kulipa shilingi 455,000 bei ambayo Profesa Muhongo aliipunguza na kufikia shilingi 177,000 kuanzia januari 2013 kabla ya kufikia bei ya sasa.

Aidha mradi wa REA umeelezwa kumng'arisha Prof Muhongo, na licha ya kujiuzulu nafasi ya uwaziri, ameendelea kukumbukwa kwa uchapakazi wake unaoelezwa kuwa ulilenga kupambana na umasikini.

Baadhi ya wananchi hasa wa kanda ya Ziwa wameendelea kumkumbuka kwa jitihada aliyofanya ya kuwapatia umeme na kuwapa ruzuku wachimbaji wadogo wa madini hali iliyowashawishi baadhi ya wazee wa kanda hiyo kumuomba awanie Urais.

"Kila unakopita mkoani Mara na mikoa ya jirani ni jina la Muhongo, wazee kwa vijana, wakazi wa maeneo ya vijijini hawakupata kujua umeme wa majumbani hadi muhongo aliposhika uwaziri wa Nishati, kwa hiyo inawauma ni kwa kosa lipi aliamua kujiuzulu, wana usongo kweli na wale wote waliomfanyia fitina, toka wanasiasa, wabunge na matajiri", ameeleza Bwana Ayoub aliyekuwa mikoa hiyo hivi karibuni.

Wakati hayo yakijiri, Profesa Muhongo ametoa maoni yake yanaoonesha kuwa ya kizalendo kwa watendaji wa serikali pamoja na kushauri juu ya mwelekeo na dira ya nchi kwa mustkbali ujao kwa kutilia mkazo katika kilimo.

Katika maoni yake aliyoaita, Tanzania ijayo: Uchumi wa gesi kutoa mtaji mkubwa kwa kilimo cha kisasa, Profesa Muhongo ametaja vitu muhimu vya kuboresha kilimo ili kukidhi matakwa makuu matatu.

"Ardhi, maji, raslimali fedha, pembejeo za kisasa (vitendea kazi), zikiwemo trekta na mbolea, raslimali watu – wakulima, elimu ya kilimo bora, wataalamu – sayansi, teknolojia na ubunifu pamoja na taasisi zake", ameandika katika maoni hayo yaliyosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.

Amesema nchi iwe na wataalamu au wanasayansi wa kutosha wa tabia nchi na aina ya mbegu na ubora wake (climate and seed scientists) pamoja na viwanda vya mazao ya kilimo, masoko ya ndani na nje ya nchi, sera na sheria za kuimarisha kilimo kidogo na kikubwa kwa mazao ya aina zote.

Aidha akielezea mahitaji ya chakula wakati nchi inapata Uhuru Mwaka 1961, amesema Dunia ilikuwa na jumla ya wakazi bilioni 3.08, 1971 (bilioni 3.77) wakati mwaka 1990 ilikuwa na bilioni 5.28, mwaka 2000 bilioni 6.10, mwaka 2010, bilioni 6.89 na Mwaka 2013 bilioni 7.13.

Amesema Tanzania itakapokuwa nchi ya kipato cha kati mwaka 2025, Dunia itakaliwa na watu bilioni 8.1 na itakapofikapo 2050 idadi ya watu inakisiwa itafikia bilioni 9.6, na kwamba idadi hiyo inakadiriwa kufikia bilioni 10.9 itakapofikia Mwaka 2100.

"Watu wote hawa watahitaji chakula cha kutosha kuepuka baa la njaa", ameeleza Profesa Muhongo na kusisitiza kuwa hata katika vitabu vya dini anatajwa nabii mmoja aliyeitahadharisha jamii yake na janga la njaa hivyo aliwataka watu wake walime sana na kuhifadhi chakula kwa ajili ya kipindi kigumu kilichofuata baadaye.

Akielezea umuhimu wa mazao ya chakula ameshauri kilimo kijielekeze kuzalisha aina ya vyakula ambavyo Dunia inahitaji kwa wingi.

"Isitoshe asilimia 85 ya kilimo chetu ni cha mazao ya chakula (food crops). Kwa mfano, uzalishaji wa mchele Duniani kwa Mwaka 2014/15 unakadiriwa kuwa tani milioni 496 huku matumizi ni tani milioni 500", ameandika Profesa Muhongo katika makala hiyo.

Aidha ameyataja Mazao 10 yanayolimwa kwa wingi na kulisha Dunia mbali ya mahindi, kuwa ni pamoja na mchele, ngano, viazi mviringo, mihogo, soya, viazi vitamu, viazi vikuu, mtama na ndizi mzuzu (plantain).

"Nchini China, zaidi ya hekta milioni 30.2 za ardhi yenye rutuba nzuri imetengwa kwa ajili ya kilimo cha mahindi, lakini Mwaka 2011, kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 14, China ilinunua mahindi kutoka nje; na inakadiriwa kwamba itaagiza mahindi ya kiasi cha tani milioni 15 kutoka Marekani peke yake. Japan ndiyo nchi inayoongoza kwa kununua mahindi kutoka nchi nyingine kwa kiasi cha takribani tani milioni 16 kwa mwaka", ameandika Profesa Muhongo.

Aidha ameeleza kuwa mtaji mkubwa wa kilimo utapatikana kwenye uchumi wa gesi asilia ambapo kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya KILIMO cha Tanzania, Uchumi wa Gesi Asilia (ambao ni mpya) utalazamika kutoa fedha za kuwezesha kupatikana kwa wingi na kwa ubora mkubwa nyenzo muhimu na kusisitiza kwamba Uchumi wa Gesi ndiyo INJINI KUBWA na MPYA ya kutumika kufuta umaskini nchini Tanzania.

"Gesi Asilia ni Umeme kwa Kilimo cha kisasa na Viwanda vyetu, Gesi Asilia ni Mbolea ya Mashambani, Gesi Asilia ni chanzo kikubwa na cha uhakika cha Raslimali Fedha kwa kilimo chetu cha kisasa (vikiwemo viwanda vya mazao ya kilimo - agricultural industries) ambacho kitavutia na kutoa ajira kwa Watanzania wengi", ameandika.

Aidha amesema Ushirikiano na mpangilio unaotekelezeka vizuri kati ya Uchumi wa Kilimo na Uchumi wa Gesi Asilia, Viwanda na Huduma (services) ndio utakaokuza uchumi kwa zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka, kutokomeza umaskini na kuwaandaa watanzania wawe nchi ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025.

Wakati huohuo, Msomi na mwanataaluma ya uhasibu na usimamizi wa fedha, Salim Khatr ameipinga vikali ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Bwana Zito Zuberi Kabwe(PAC) ambayo ilichunguza akaunti ya Escrow, kuwa haikuwa yenye ukweli mtupu.

"Ripoti ya PAC iliyowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa PAC, Mh. Zitto Kabwe mwezi Novemba 2014 ilijaa uongo, udanganyifu na ulaghai wa kiwango cha juu kabisa. Ripoti ya PAC ina sifa zote za kuitwa "Utapeli wa Kisiasa", ameandika mtalamu huyo.

Aidha amesema Kamati ya PAC ilitumia mseto wa hoja zilizochanganywa kwa makusudi licha ya kujua kuwa suala la mgogoro wa IPTL na TANESCO uliopelekea kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta lina mambo mengi kama mahakimu wa kesi ya ICSID namba ARB/10/20 walivyolezea kuwa na "complex facts, multiple proceedings and multiple participants".

"Utaalamu wa kuchanganya mseto wa hoja kwa nia ya kuwachanganya na kuwahadaa walengwa unaweza kuvumilika kisiasa. Lakini uongo na udanganyifu katika kutoa "facts" za uongo na kutoa nukuu za uongo haziwezi kuvumilika sehemu yoyote ile", ameandika mtaalamu huyo katika makala yake" UONGO WA TAARIFA YA KAMATI YA PAC KUHUSU SAKATA LA ESCROW.

Kwa ajili hiyo, tuhuma zote za Ripoti ya PAC ni za UONGO kwa kile kilichoelezwa na Msomi huyo kwa kuangalia barua yenye kumbukumbu Na. SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 ambayo ni barua yenye kurasa tatu isiyo na maneno yoyote siyo tu yanayoweza kutafsiriwa kama ilivyonukuliwa na Ripoti ya PAC bali haina maneno yoyote yanayokaribiana na maana ya maneno yaliyonukuliwa na Ripoti ya PAC hivyo kuwa ya UONGO.

Kuhusiana madai ya PAC dhidi ya Profesa Muhongo makala hiyo imeandika kwamba picha iliyojengwa kwenye Ripoti ya PAC ni kuwa Prof. Muhongo alimuita Rugemalira na Sethi ofisini kwake.

Imedaiwa kuwa Rugemalira aliambiwa apeleke kiasi cha fedha anachotaka kulipwa na Sethi pamoja na ushahidi kwamba amenunua Hisa 7 za Mechamar katika IPTL, hivyo Wakakutana wote watatu ofisini kwa Prof. Muhongo na biashara ya kuuziana hisa ikafanyika hapo ofisini kwa Waziri.

"Hayo ni madai ya UONGO kwa kuwa nukuuu ya "Mkataba wa Mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP" ) yanayodaiwa kuwa ndiyo "uthibitisho" wa madai hayo kwa makusudi kabisa yalichakachuliwa kwa lengo la kumuhusisha Profesa Muhongo", imedaiwa.

Ilifanywa hivyo ili kukamilisha malengo ya kisiasa na kutimiza matakwa ya wanaosemekana kuwa nyuma ya mpango huo kwa kumtumia mtoa hoja binafsi mbunge Bwana David Kafulila.
 
....aende huko huko akawaibie, huku hatumtaki. kwanini akomalie bongo kama anauwezo wa kula shavu viwanja...? anajua alichokuwa anapata bongo kwa wizi, kwa wazungu hawezi kuwaibia bhabhabhaaaaaaabaaaa....
 
Reactions: BAK
Hela alizoiba zikiisha hutamsikia tena
 
Kwa mfumo wa ndg zangu waTZ (juu ya kusoma) sidhani kama wengi watasoma hiki kitabu chooote ulicho_post hapa. Ngoja waje tuone.
 
Anazidi kung'ara kwa kuwapa maelezo vijana wake LUKU isipatikane......
 
Reactions: BAK
Hivi hizo gharama ni za kweli au mbwembwe tu?
 
Huyu bwana arudi tu next year kufanya kazi, atakua amejifunza kuacha dharau na majigambo yasiyokwisha... he is hard working and intelligent, dharau ndio iliyomponza, sidhani kama alikula escrow
 
mimi hakuna watu nawadharau kama wasomi wa Tanzania watumiwa na ccm kama toilet paper.

wananchi hawana matumaini na hawa wasomi uchwara,wasomi wasio na msaada kwa nchi yao, wasomi weeeeezi!,wasomi wasio na mipango!!!bendera fata upepo!!!! wasomi ambao hawana umuhimu kabisa!!

NCHI YETU IMEYUMBA MNASHANGIRIA TU!!!!
MISINGI YA NCHI IMEHARIBIKA!!!
 
Nillifikiri amepata post nyingine ya kimataifa, manake nyota yake ipo huko na sio kwenye siasa!
 

Hao wananchi waliokupa maoni yao ni wangapi na wa wapi maana wapo pia wanomkubali Muhongo kwa kuona kwa macho yao umeme uliofika katika vijiji vyao. tuache kuzisemea nafsi za watu ambazo hatuzijui tuzisemee nafsi zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…