Prof. Mbarawa abaini Madudu miradi ya Bwana na Umwagiliaji Meatu

BUSAMUDA

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
612
358
Prof. Makame yupo ziarani katika mikoa ya Geita na Simiyu. Leo tarehe 21/12/2015 akiwa wilaya Meatu ambapo aliingia mida ya saa 5 Asubuhi baada kunyetishwa Taarifa ya Mradi wa Bwawa kwa ajili ya matumizi ya Binadamu lililojengwa katika kijiji cha Mwanjolo na kugharimu karibu bil. 1 bila KUKAMILIKA na mkandarasi kutimua mbio na mradi wa Umwagiliaji uliojengwa katika kijiji cha Gwila uliogharimu karibu Bil. 1 bila KUKAMILIKA na mkandarasi kutimua mbio.
Prof. Alifunga safari kwenda kuiona miradi hiyo ili achukue hatua mnamo saa 8 mchana lakini safari hiyo ilikatishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kuziba daraja, hivyo msafara huo kushindwa kuvuka.
Hata hivyo Prof. Huku akionesha hali ya kukasirishwa ameahidi kurudia ziara hiyo ili aione miradi hiyo.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom