Prof: Maghembe atamani mauti yamkute mpinzani wake

Sep 26, 2013
33
10
ndugu wadau
hayo yalibainika hivi karibuni kwenye kikao cha kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Mwanga na Ujumbe toka kamati ya Usalama na Maadili ya CCM makao makuu.

Kwamba siasa za makundi mawili hasimu ya Profesa Maghembe ambaye ni Waziri "Mzigo" wa Maji na Mbunge wa jimbo la Mwanga(Mzigo - kwa mujibu wa katibu wa Itikadi na uenezi Bw. Nape Nnauye) na Mwanasheria wa Kampun ya Trust Mark attorney ya Jijini Dar es salaam ambaye amewahi kugombea Ubunge jimbo hili na sasa ni MNECCCM kupitia Wilaya ya Mwanga Ndugu Joseph Tadayo zimefikia hatua mbaya kiasi ambacho timu ya Mheshimiwa Mbunge imefikia hatua ya kutengeneza mazingira ya kumtoa roho mpinzani wake kwa njia mbali mbali ikiwemo ushirikina au kumkodishia majambazi.

paper work ya mpango huo hatari na usiokuwa na hata chembe ya siasa za ushindani tayari umeshatua makao makuu ya CCM baada ya kutolewa kama ushahidi kwenye kikao hicho ambacho mheshimiwa Mbunge alijaribu kukimbia mara tatu kukwepa shutuma kutoka kwa viongozi wenzake wa CCM wilaya na Mkoa wa Kilimanjaro ambao walikuwa ndani ya Kikao hicho. Majaribio yote ya kutoroka ndani ya ukumbi wa Mikutano wa CCM yaligonga Mwamba baada ya Katibu wa CCM Mkoa kilimanjro Bwana steven kazidi kumkomalia asijaribu kutoka ndani ya kikao hicho kwani kutoka kwake kijeuri kutasababisha waongeze kuni moto uliokwisha washwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye kuwa Prof. ni Mzigo kwani bado wana nyaraka nyingi za kuthibitisha kuwa ni mzigo pia ndani ya Chama Mkoa wa Kilimanjaro.

Akijibu shutuma hizo alisema watu hasa Kazidi hawana Shukrani kwani yeye alifanya jitihada kwa Bwana kazidi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Kahawa wakati yeye akiwa Waziri wa kilimo sasa anapata vipesa ndo vina mpa jeuri ya kumzushia na kumchonganisha na Mwenyekiti wake wa CCM Taifa ambaye kwake ni kama kaka.

Anasema mbinu zote za kumtoa Uwaziri zimeshindwa tangu zamani ndo maana wanamtengenezea mazingira mabovu ili wakina Kinana wapate nguvu ya kumsulubu jaribio ambalo litashindwa kwani yeye na Mwenyekiti hawakujuana kwenye majukwaa ya siasa.

Huyo ni profesa maghembe wa CCM
naomba kuwasilisha
 
Hapa Jukwaani hapatakiwi majungu...unajua hilo?

Ukiombwa ushahidi wa haya uliyoyasema utaleta?
 
Hapa Jukwaani hapatakiwi majungu...unajua hilo?

Ukiombwa ushahidi wa haya uliyoyasema utaleta?
upo wa kutosha! ingawa hapa sio mahakamani lakini unaweza kwenda kjiridhisha mwenyewe kwa kuwahoji wanamwanga na viongozi wao walikuwa kwenye kikao hicho. na wala sio siri. Magamba tunajua ni magaidi kutoa roho za watu ni kama vile kuua mdudu chawa! Upo Mkuu
 
asimwogope tadayo, hofu yake angeipeleka kwa Henry kilewo wa chadema huyu ndo atakayemtoa huyu majembe
 
Back
Top Bottom