Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Kama tutakumbuka mnamo tarehe 19 Mwezi Februari, 2016 Rais Dkt. John Magufuli, amepiga marufuku uagizaji na uingizaji sukari kutoka nje ya nchi kuanzia jana akiwataka watendaji wa Serikali, kutotoa vibali vya kuingiza bidhaa hiyo.
Rais John Pombe Magufuli alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari kuingia nchini, vibali atavitoa yeye si mtu mwingine yeyote ili kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.
Rais Dkt. Magufuli aliyasema hayo Ikulu, Dar esSalaam, jana wakati akitoa shukrani zake kwa waandishi wa habari, wasanii na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015. Baada ya tamko hilo Serikali ilitangaza bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo nchi nzima.
Rejea kauli ya rais kupitia video hii:
================================
Mapema leo May 13 2016 aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF kama ya kukaa pembeni kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana Oktoba, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la sukari katika ofisi za chama cha CUF.
Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kuruhusu uingizaji wa sukari kutoka nje kwasababu viwanda vyetu vya ndani vya sukari havitoshelezi mahitaji ya sukari kwa wananchi na pia amesema vimesimama kuzalisha sukari kwa zaidi miezi sasa.
Prof. Lipumba amesema TAKUKURU badala ya kuwakamata Tegeta Escrow Account walio kwapua mabilioni ya fedha za umma lakini maajabu ni kwamba sasa TAKUKURU wanashughulika sasa na wanaoficha sukari, takwimu za wizara ya kilimo zinaeleza, nchini hakuna sukari ya kutosha lakini watu wanashughulika na kuitafuta sukari
Prof. Lipumba akaongeza pamoja na msako mkali sukari iliyokamatwa nchi nzima haifiki tani 10000 lakini kwa kuwa Rais ameshasema sukari imefichwa viongozi nao wanarudia kauli hiyo kuwa sukari imefichwa yasije yakawakuta yaliyomsibu mama Anne Kilango Malecela ambaye alitolewa katika nafasi ya ukuu wa mkoa baada ya kuonekana amepotosha taarifa za idadi ya watumishi hewa kwa mkoa wa Shinyanga.