Prof. Lipumba: ACT-Wazalendo imeongeza damu yenye virusi ikidhani ni damu salama

Yeye ametaka kua mwenyekiti wa msajili na wa kisutu amekua lakini haishiwi maneno hakika jamaa ameumia sana yani ni sawa na kutaka kumfukuza kazi mfanyakazi wako ofisini kabla hujafanikiwa mfanyakazi anahamia UN
Hahaa jamaa kapigwa K.O alidhani kuwa fitina aliyoifanya itammaliza mwenzie " Bahati mbaya amekuja kushtuka kuwa kumbe alikuwa amempiga chura teke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiwa TBC leo asubuhi mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ameisikitikia na kuishangaa sana ACT kwa kitendo walichokifanya cha kumpokea Maalim Seif na wafuasi wake.

Akifafanua jambo hilo Lipumba amesema ACT ilichokifanya na sawa na mgonjwa mahututi kuongezewa damu yenye virusi ambaya lazima imuue.

Lipumba amedai kwamba Maalim Seif ni damu yenye virusi ndani ya ACT hivyo ACT wajiandae kufa kifo kibaya sana.

Pia Lipumba amemfananisha Maalim Seif na Mrema na amedai kwamba CUF ipo na itaendelea kuwepo milele.

Lipumba amewaomba wana CUF wasiyumbishwe na kitu chochote kwani yeye kama mwenyekiti wao yupo imara sana

Ahaa haa
huyu mzee ana maneno kweli du.
 
Wanasiasa hawaishiwi maneno
Mimi nadhan ACT itaongeza wabunge wengi zAidi bara na visiwani. Atakae angamia ni yeye.
Hebu atie mguu zanzibar na
Pemba aone moto wake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotazama TBC kwa hoja kuwa eti ina boa, hadi wengine kuuita TBCCM, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kwa kuangalia TBC. Mimi naangalia TBC japo nina kaugomvi kidogo na wife hapa kuhusu hili, yeye anataka kuangalia Clouds 360, hivyo sometimes lazima ubaba utumike kinguvu, TV ya kuangaliwa na baba ni TBC!, hivyo mtu kuwa mzalendo wa kweli wa taifa lako, ni pamoja na kuiangalia TV ya Taifa lako, hata kama ni kweli sometimes inaboa, uzalendo ni kuweka utaifa mbele, hivyo TV ya Taifa ndio TV yetu sisi wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo tunaangalia TBC.

Leo Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
kwanza ulivyotumia tu msuli mkubwa kuipamba hiyo tbc,huyo mama anaakili ni mzalendo zaidi mwachie tu 360 yake.hiyo channel tbc huwa siangalii,ilajuzi kati aisee ilinilazimu kifurushi kilipoisha,kwa hasira ikabidi niuze gunia la mahindi nikanunue kifurushi niachane na hako kaugonjwa ka tbccm
 
Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.
Pascal nyooka sema hivi Lipumba anatumiwa na Serekali inayoongozwa na ccm kuvuruga CUF sijaona kosa la Lipumba
 
data na wewe🎶🎵
tipwatipwa tetema shuka chini tetema oomama tetema..
haya twende tetema.. ooomama tetema..
yani kama umepigwa SHOTI... tetema
nipe migandisho ya robot. tetema..
ukutani mpaka kwenye KOCHI.. tetema
Kwenye GIZA mama SHIKA tochi... tetema.. aiii..
KATOTO KAMENOOGAAA.. OOMAAMAA..
NIKUPE ndidhi dha BUKOBA.. oomama...
nakapandisha BODABODA.. Oomama..
kakichoka kuchuma mboga... Ooomama

KONK.. FAYA.. LIQUIDY.. Nikunyonge ka ZIGIZIG:p:p:p:p:p
 
Jana nilikuwa nimekaa na Waziri pamoja na afisa mkubwa wa TIS. Waziri ni rafiki yangu. Nikamwuliza,
SWALI: Ebu niambie ukweli kabisa, maneno haya yanayotamkwa kuwa mgogoro wa CUF umeletwa na CCM, ni kweli?'
JIBU: Huo ndio ukweli
SWALI: Kwa kilichotokea sasa, yaani kwa maana ya alichokifanya Seif, bado mnaona mmefanikiwa?
JIBU: Kwa kiasi fulani tumefanikiwa
SWALI: Nionavyo mimi ni kama hamjafanikiwa kwa maana kwa sasa Lipumb anaweza kuwa Mrema. Na ikiwa hivyo halafu ACT ikawa na nguvu kushinda hata CUF ilivyokuwa mwanzo, hamwoni ninyi mtakuwa mmesaidia zaidi kuujenga umoja wa wapinzani? Zamani CUF na CDM hawakuwa wanakaa pamoja, wala CUF haikufikiria kuungana na CUF. Leo ACT imeungana na CUF, Lipumba hana CUF, ana makarayasi ya CUF. Leo vyama vya upinzani vyote vimekuwa na umoja kutokana na madhira yanayofanana - dhulma inayofanywa na CCM dhidi yao, wewe unasemaje? Huoni kama ni miscalculation ya hali ya juu?
JIBU: Unachokisema kuna ukweli mkubwa.
Mkuu Bams. naunga mkono hoja, ACT inaweza kuwa stronger kuliko CUF tatizo kwangu ni mafahali wawili hawawezi kuka zizi moja, kwa vile Zitto ni very calculating, anajua anachotafuta kwa kumkaribisha Seif, lazima akubali kuwa mdogo, akabidhi chama na madaraka yote kwa Maalim, yeye asubiri tuu mavuno.
P.
 
Pasko kwa vijana tutafaidika nini na kauli za Lipumba? Vijana tunataka ajira na njia mbadala za kukuza uchumi. Wenzetu Kenya na Rwanda wamezindua magari yao sisi tupo bussy kujadili Lissu Lipumba na mengineyo ya kusadikika. Tuwaache wafu wazike wafu wao. Tangalie namna ya kujikwamua ktk mfumo huu hasi wa kiuchumi. Nawaza tu hivo. TBC kwangu nilishaifuta kabisa ktk list of channels


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. Lipumba anasisitiza ofisi za CUF nchini kote ni mali ya chama cha CUF na sio mali ya mtu, hivyo amelaani kitendo cha watu kupora ofisi za CUF na kuzigeuza ni za ACT, amesema atazipigania ofisi hizo ambalo ni mali halali ya CUF, lazima zibaki CUF.
Oooh basi kwa mtindo huu huu turudishieni kumbi na viwanja vyote vya mipira vinavyomilikiwa na fisiem nchi nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotazama TBC kwa hoja kuwa eti ina boa, hadi wengine kuuita TBCCM, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kwa kuangalia TBC. Mimi naangalia TBC japo nina kaugomvi kidogo na wife hapa kuhusu hili, yeye anataka kuangalia Clouds 360, hivyo sometimes lazima ubaba utumike kinguvu, TV ya kuangaliwa na baba ni TBC!, hivyo mtu kuwa mzalendo wa kweli wa taifa lako, ni pamoja na kuiangalia TV ya Taifa lako, hata kama ni kweli sometimes inaboa, uzalendo ni kuweka utaifa mbele, hivyo TV ya Taifa ndio TV yetu sisi wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo tunaangalia TBC.

Leo Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali

Nendeni kazini Paskali wewe na dada yangu...

Hii tabia ya kunyang'anyana rimoti badala ya kwenda kuhemea mlo wa watoto, si poa...

Mwacheni Prof Lipumba ajilipe malimbikizo ya ruzuku na huo ndiyo mwanzo na mwisho wake....

Mission accomplished (By Chakubanga)
 
tipwatipwa tetema shuka chini tetema oomama tetema..
haya twende tetema.. ooomama tetema..
yani kama umepigwa SHOTI... tetema
nipe migandisho ya robot. tetema..
ukutani mpaka kwenye KOCHI.. tetema
Kwenye GIZA mama SHIKA tochi... tetema.. aiii..
KATOTO KAMENOOGAAA.. OOMAAMAA..
NIKUPE ndidhi dha BUKOBA.. oomama...
nakapandisha BODABODA.. Oomama..
kakichoka kuchuma mboga... Ooomama

KONK.. FAYA.. LIQUIDY.. Nikunyonge ka ZIGIZIG:p:p:p:p:p


😁😁😊😊😊😊
 
Back
Top Bottom