Prof Lipumba amvaa Rais Samia, asema kuna watu wanamtengenezea ajali kisiasa

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,757
Mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba amemvaa Rais Samia kutokana na madudu yaliyomo kwenye mkataba wa ukodishwaji wa bandari za Tanzania kwa kampuni la DP world kutoka Dubai kwa haufai na huenda kuna watu ndani ya serikali wanamtengenezea ajali kisiasa ili ashindwe kwenye uchaguzi ujao.

Prof Lipumba amesema alikuwa anampigia debe Rais Samia atwae tuzo ya Nobel lakini kwa madudu yaliyomo.kwenye mkataba wa DP world haitawezekana tena kutwaa tuzo hiyo.


 


Mzee Lipumba bwanaaa.....

Wataalamu wetu wameshatudadavulia kuwa DP WORLD wanakwenda kutupatia nusu ya bajeti ya nchi ya "fiscal year".....

#MamaAnaupigaMwingi


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Bibi anapaishwa kama unyoya,siku inakuja atadondoka na kupasuka kama nazi!
 
Huyu mtu wa hovyo sana anaacha kumpa makavu live anazunguka kama jogoo anayemendea mtetea... alikua wapi kabla ya azimio la bunge?

Huyu nae ni wale wale ambao akili zao zimeunganikana na utumbo hivyo fikra hutegemea kichwani kuna nini... huyu ndo alimtolea JK dirishani 2010.

Vipi hawajampa pilau? Maana na usomi wake akiona pilau ulimi humcheza mithili ya nyoka aliyefyonza yai na macho huangaza mithili ya mamba!

Sio wa kumuamini huyu!
 
Hivi kwa mkataba huu maanake TPA haipo tena au ??!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…