Prof Lipumba ajishusha, amuomba Seif aiondoe kesi mahakamani wafanye mazungumzo.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,376
24,928
Profesa Ibrahim Lipumba amemuomba Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuondoa kesi mahakamani ili wafanye mazungumzo ya maridhiano.



full_size_20170208102640.jpeg


LIPUMBA AMTAKA MAALIM SEIF KUFUTA KESI
LIPUMBA-NA-SEIF-720x375.jpg

Profesa Lipumba, katika mahojiano yake na Tido Mhando wa kituo cha televisheni cha AZAM, amemuomba Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kuondoka kesi Mahakamani ili wafanye mazungumzo ya maridhiano wakati alipoulizwa kuhusu suluhisho la mgogoro uliopo ndani ya chama hicho.

Akijibu swali hilo, Lipumba alisema kuwa cha kitakacholeta suluhu ni mazungumzo kati yao kwa sababu wao ni wanasiasa wakongwe na wametoka mbali. Alisema kuwa kama waliweza kusuluhisha na kupata mwafaka wa mgogoro mzito kati ya CCM na CUF, na huu uliopo ndani ya chama chao pia unaweza kumalizwa bila kutumia Mahakama.

“Suluhishsho ni sisi kuzungumza. Maalim Seif alizungumza kwenye mgogoro wa Zanzibar kutafuta mwafaka kwa kumshirikisha Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, iweje mimi Mwenyekiti wake ambaye tupo pamoja muda mrefu tusifanye mazungumzo tufikie muafaka?,” aliuliza Lipumba

Profesa Lipumba alisema kuwa yeye ni Mwenyekiti halali wa chama hicho ambaye alichaguliwa na mkutano halali na kwamba Katibu Mkuu wake ni Maalim Seif Shariff Hamad tangu mwaka 2014.

Kuhusu UKAWA, Profesa Lipumba alisema kuwa umoja huo ulikuwa na lengo la kuutetea rasimu ya Katiba ya wananchi lakini baadae wakasema wafanye majadiliano mengine ya kisiasa lakini CHADEMA kiliwahadaa vyama wanachama wa umoja huo kwa kutumia utaratibu wa kuwaondoa kisiasa washiriki wenzao.

Chanzo: Swahili times
 
Binafsi nachukia haya mazungumzo, mazungumzo mazungumzo! Mnazungumza nini sasa? Kwanini asingefanya mazungumzo kabla hajatenda? Umetenda na kukosea halafu unaomba mazungumzo.
 
Huyo ni msaliti tu hapaswi kupewa nafasi tena, aende huko ccm wakamkate mkia
 
Msaliti mkubwa yule! Asubiri kesi iishe, mshindi achukue kila kitu; Winner takes it all!
 
Back
Top Bottom