Kitila aliitembelea mitaa mbalimbali ya kata hiyo kunadi sera, kueleza aliyotekeleza, kusema atakayofanya akishinda, kusikiliza changamoto na kutoa majibu ya suluhu zake.
Katika kuendelea na kampeni hizo Kitila alikutana na mabondia ambao pia ni wafanyabiashara katika soko la Ndizi Mabibo na kuwasikiliza huku wakimueleza kuwa wanahitaji kuungwa mkono ili kuweza kuwa na sehemu ya mazoezi/mafunzo itakayowasaidia.
Kitila aliahidi kuwasaidia akieleza kuwa fedha za kwanza atakazopewa za mfuko wa jimbo atawakumbuka mabondia hao.
Jumatano ya Septemba 24, 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CCM Professa Kitila Mkumbo Kitila Mkumbo ameendelea kupambana kulinda kazi yake ya ubunge kwa kusaka kura kwa udi na uvumba katika Kata ya Ubungo.
Kitila aliitembelea mitaa mbalimbali ya kata hiyo kunadi sera, kueleza aliyotekeleza, kusema atakayofanya akishinda, kusikiliza changamoto na kutoa majibu ya suluhu zake.
Katika kuendelea na kampeni hizo Kitila alikutana na mabondia ambao pia ni wafanyabiashara katika soko la Ndizi Mabibo na kuwasikiliza huku wakimueleza kuwa wanahitaji kuungwa mkono ili kuweza kuwa na sehemu ya mazoezi/mafunzo itakayowasaidia.
Kitila aliahidi kuwasaidia akieleza kuwa fedha za kwanza atakazopewa za mfuko wa jimbo atawakumbuka mabondia hao.
Kwa upande wa Mama lishe wanafanya biashara eneo hilo waliomba kuwezeshwa na wao kuweza kutumia nishati safi ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ajenda ya nishati safi.
Pamoja na mambo mengine Kitila alimuombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan, alijiombea na yeye kura na kumuombea mgombea udiwani wa kata hiyo Jaffary Nyaigesha.