Prof J jaribu kuwaelemisha wenzako maana ya kodi badala ya kuwasemea bungeni

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
4,601
Jamii Forums Mods Naomba hii Thread isiunganishwe ha zingine please.

Nimeiona video wakati Mbunge Joseph Haule akizungumzia jinsi Diamond na Ney wanavyodaiwa na TRA. Na nimeshangaa kuona Diamond anampa shavu na kuisema CCM kiaina kama vile alifanya ile kazi ya kuwaimbia CCM kwa mapenzi ya nchi.

Nijuacho mimi Diamond aliajiriwa na CCM katika ile kampeni na alilipwa kama alidhani alimpigia kampeni rais akwepe kodi basi alichagua chaguo baya. Nauungana sana na Mh Haule kuwa mtetezi wa wasanii maana ndiyo kazi moja wapo ya mbunge kuwasemea wananchi bungeni lakini pia ajue kuwa anatakiwa kuwapatia hao anaowatetea elimu ya kodi.

Jumapili wiki hii gazeti moja la hapa UK lilitoa list ya mabilionea, katika mijadala ya TV walisema hii ni nzuri lakini ubaya wake ni kwamba itawaibua watu wa Tax kuwachimbua hawa jamaa.

Nikirudi kwa kina Diamond, hawa jamaa kila kukicha wanatoa maytangazo mpaka katika Facebook kuwa watu wa kwanza ku comment watapewa elfu kumi, mara wanaonyesha mpaka nyumba wanazozimiliki nje ya nchi wanashau kuwa makao yao ya kodi yapo Tanzania. Kuna video alionyesha matumizi aliyoyatumia alipokwenda katika safari ya ulaya ya mwaka juzi alisema alitumia dola 50,000.00 najua kuwa ana uwezo lakini tatizo la wasanii wengi hawajaenda shule na zaidi ya hapo wanaajili rafiki zao ambao elimu zao za Kibashite.

Duniani kote watu wa kodi wanafurahi sana unapowakea njia rahisi kwa kuanika utajiri wako. Watu wenye busara huwa wana ma accountant wa maana kwa kutunza hesabu zao. Kama una kitu kinaitwa wasafi label na hujasajili kama private entity ina maana kodi yako wewe itakua ya kukadiriwa tu maana huna vitabu vya hesabu. Na inawezekana vipi uwe na mpaka uwezo wa kuuza vitu online lakini huna vitabu vya maana vya mahesabu yako???? Ili kodi yako ijulikane na isiwe ya kudariwa unatakiwa uwe audited na registered Auditor halafu peleka return zako serikalini ili wa kukadirie kufuatana na faida yako uliyoipata katika kipindi hicho cha fedha.

Lakini wadogo zetu wanaona kazi kutumia pesa kukodi watu wenye utaalamu kuwasaidia na kuwashuri wanashinda wakishindana nani anamiliki magari na nyumba za maana. Nakumbuka wakati nikiwa mwanza kuna kijana mmoja nadhani alipata pesa za madini na akaanzisha ile hotel ya rock Beach. Alianza kujenga bila mkopo wa bank na tulimsihi sana kuwa TRA watamsifilisi asipokuwa mjanja. Akatuuliza ujanja gani tukamwambia aende Bank anakoweka pesa akakope pesa za ujenzi wa nyumba ili Zakayo akija apate kisingizio.

Diamond acha kulia tafuta wataalam wakague vitabu vyako ili ijulikane kila mwaka unapata faida gani halafu peleka TRA na vithibitisha ama siyo jamaa wakija wana sharia ya kukagua na wakiona umefanya makosa wanachukua faini ya mwaka huo wanarudi nyuma miaka mitano na hiyo ni sheria sema tu longolongo ya miaka ya nyuma iliwadanganya wengi.


Prof Jay waelimishe wenzako kama na wewe unaelewa.....

 
Back
Top Bottom