longi mapexa
JF-Expert Member
- Jul 18, 2015
- 3,197
- 3,994
Hapa sasa nimeona hata umuhimu wa degree yangu.Tumemwelewa na tunaondoka na dondoo zifuatazo;
Kwanza ni lazima tuanzie kwa mwandishi mwenyewe ambaye ni known Pan Africanist ambao misimamo yao ipo dhahiri kuhusu Western & Company.
(a) Pili kaelezea jinsi NATO ilivyojipanua kumzunguka Urusi, ( muhimu zaidi kuzuia Ujerumani kuwa mshirika wa karibu wa Urusi, hawa watatengeneza very powerful alliance ~ kutokana na huu mzozo, US kafanikiwa kutengeneza gape kati ya Ujerumani na Urusi tofauti na miaka iliyopita.
(b) Tatu ni kuwa, tunavyomshtumu Urusi kuivamia Ukraine hivyo hivyo tunapaswa kuilamu NATO kujisogeza karibu na Urusi. Hoja ya msingi hapa ni kuwa, hivi vita vinachangiwa kwa upande mmoja na Urusi kujaribu kujipanua nje ya mipaka yake ili kukabiliana na upanuzi wa NATO (Both NATO and Russia are wrong, kwa mtizamo wake).
(c) China anataka kuwa taifa kubwa kiuchumi na anaihitaji Ulaya ili kufanikiwa, hivyo haoni Mchina akijitumbukiza katika masuala ambayo yataathiri ndoto zake.
Hoja ambayo sijaikubali sana ni raisi wa Ukraine kukosa political legitimacy kwa kuwa raia wa Israeli. Katika nchi ambayo Sheria zake zinaruhusu uraia pacha sioni kama itaibua maswali kwa umma.