Prof. Baregu: Prof. Kabudi na Humphrey Polepole mkitusaliti kuhusu rasimu ya Warioba tutawashangaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,061
164,369
Prof Baregu amewataka waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba Prof Kabudi na Polepole kutosahau msimamo wao ndani ya tume.

Amesema baada ya tume kuvunjwa, yeye pamoja na Warioba, Kabudi, Butiku na Polepole waliendelea kufanya mikutano ya kuhamasisha rasimu ya Warioba chini ya mfuko wa Mwalimu Nyerere.

Amesema yeye aliamini ktk serikali moja na Warioba aliamini ktk serikali mbili lakini UKWELI waliokutana nao uliwafanya wabadilike.

Hivyo amewatahadharisha endapo wataisaliti rasimu ya Warioba, wananchi watawashangaa.Wewe unalisemeaje hili?Karibu

Chanzo: ZITV
 
Unataka usaliti upi ,unasubiri zaidi ya alioufanya pole pole juu ya Katiba mpya? Labda tusubiri kwa Kabudi n.a. Baregu.
 
Watanzania tena walio na Bahati ya kusoma kidogo Dawa yao ni ndogo sana tumbo jamani tumboooo wee tumboo,kabla haja sisitiza kuto salitiwa atafute njia ya kukanya tumbo kwanza,kwani wote hao ukweli wanaujua lakini jeee,tumbo litawaruhusu kusimamia walichokua wakikiamini awaliiii????
 
Mbona Baregu alibadili msimamo wake dhidi ya FISADI MKUU na akaanza kumtetea tena mbele ya BUTIKU??
Watu kama wewe ni wale ambao MNA akili kama bitozi serikali ikiwaambia nendeni mkatahiriwe wewe unakwenda kuomba wakuhasi sasa FISADI MKUU ndo ndani kwenye serikali tatu
 
Polepole asaliti mara ngapi tena?! Kabudi tusubiri tu kwenye majumuisho ya bajeti yake,hata mwezi hauishii tutaona rangi yake.

BAK tafadhali tupandishie ile clip ya polepole anayosema CCM inashinda kwa wizi wa kura na siku tume ikiwa huru inatoka madarakani!!
 
Kwa kuwa CCM waliwaweka wananchi pembeni kwa ajili ya kulinda maslahi yao na wao watakuwa pamoja na CCM kulinda maslahi ya chama kwa muda,maslahi yakiwaishia watakiacha chama na kurudi kwa wananchi
 
Sijawahi kumwamini mwanasiasa, na sidhani kama nitakaa nimwamini.Labda siku nikiwa mwanasiasa nitajiamini
 
Ukishapewa madaraka,umezibwa mdomo hata yeye Baregu akipewa ulaji atanyamaza.cc Kitila Mkumbo na saga la uteuzi wa wasomi
Hapo ndo siasa zinanichosha kwa unafiki wa wanasiasa.
Hajaona usaliti uliofanywa na chama chake kwa kuwapokea mafisadi walioikataa katiba mpya walipokua ccm sasa mishipa imemshupaa kwa wenzie waliopata kibarua.
Mjinga gani atakusikiliza wewe Baregu aache kumsikiliza mwajili wake serikali?
Nyambafu kabisa...
Yaani ukiona jitu zima na ma_degree yake linaongozwa na mtu aliyepata zero utaona hata elimu haina maana.
 
Pole Pole ameshapewa cheo kwenye chama sidhani kama anakumbuka mambo ya katiba mpya
Nimeshindwa kuamini mpaka litakapotokea. Kumbuka alikuwa kama mtaalam sio mwanasiasa ktk tume. Kila siku nasubiri Mjumbe yyte ktk ile tume aende kinyume na msimamo wa tume ili ni prove theory zangu binafsi kwa tume nzima.
 
Prof Baregu amewataka waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba Prof Kabudi na Polepole kutosahau msimamo wao ndani ya tume.Amesema baada ya tume kuvunjwa, yeye pamoja na Warioba, Kabudi, Butiku na Polepole waliendelea kufanya mikutano ya kuhamasisha rasimu ya Warioba chini ya mfuko wa Mwalimu Nyerere.Amesema yeye aliamini ktk serikali moja na Warioba aliamini ktk serikali mbili lakini UKWELI waliokutana nao uliwafanya wabadilike.Hivyo amewatahadharisha endapo wataisaliti rasimu ya Warioba, wananchi watawashangaa.Wewe unalisemeaje hili?Karibu source ZITV
Chadema bana,unawatisha watu wa ccm waende kinyume na chama chao?Hilo ni gumu sana,tafuteni mbinu za kuidhoofisha ccm
Huyu baregu anazeeka vibaya,mbona yeye hajishangai kumwita lowassa mwizi kwa miaka8,akaketi kwenye kamati kuu kwa nusu saa tu akampitisha kuwa mgombea urais
 
Nilikuwepo ktk mdahalo. Elimu ya muungano iko bias sana kila mtu anajinsi anauzungumzia. Nimesikia citation za Nyerere amabzo sijawai kukutana nazo ba sidhani kama zinaukweli au kutoka kwa mzungumzaji mwanamke( Hawa Shamte).
Wazungumzaji wote watatu ni wanatoa hoja za kuupinga muungano kuwa hauna legitimacy na legality lakini mwishoni wanasema udumishwe
( Unafiki- Lwaitama)
 
Mwitikio wa raia na wanafunzi upengua sana, watu hawataki kufikirisha fikra wanatak wasemewe na wanasiasa
 
Prof Baregu amewataka waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba Prof Kabudi na Polepole kutosahau msimamo wao ndani ya tume.Amesema baada ya tume kuvunjwa, yeye pamoja na Warioba, Kabudi, Butiku na Polepole waliendelea kufanya mikutano ya kuhamasisha rasimu ya Warioba chini ya mfuko wa Mwalimu Nyerere.Amesema yeye aliamini ktk serikali moja na Warioba aliamini ktk serikali mbili lakini UKWELI waliokutana nao uliwafanya wabadilike.Hivyo amewatahadharisha endapo wataisaliti rasimu ya Warioba, wananchi watawashangaa.Wewe unalisemeaje hili?Karibu source ZITV
Usalitiwe Mara ngapi
 
Back
Top Bottom