Nadhani ungebadilisha heading sio Prof Baregu aivuruga CHADEMA ila ingeleta maana kama ingesomeka CHADEMA WAMVURUGA PROF BAREGU .
Huyu Mzee Prof Baregu anatumia muda wake na akili zake alizojaliwa na MUNGU kusaidia kupata Katiba mpya na sio hao CHADEMA wanaotaka Public sympathy ili waende Ikulu !
Narudia tena Mwaka 2015 CHADEMA wakiingia Ikulu mnichome moto nikiwa hai !
Tutakupata wapi tukuchome moto ukiwa hai ilhali hata sasa umeshakufa. Ubongo uliokufa hautoi nafasi kwa mwili kuwa mzima.
CDM hawalilii public sympathy na ndio maana huoni viongozi wakijiangusha majukwaani. CDM inalili haki yako wewe usiyejua kuwa tembo unaowaona leo na kujivunia hata watoto na wajukuu zako nao wana haki ya kuwaona.
CDM wanataka kumsaidia shangazi yako na binamu zako uliowaacha kijijini kupata huduma za afya na sio fedha zikanunue kiwanja cha makaburi ya viongozi ambao dhahiri hawatazikwa hapo.
CDM wana dhamira ya dhati ya kuona usawa unapatikana katika matumizi ya rasilimali za nchi na sio akiumwa mkamata tembo akatibiwe India ila akiumwa shangazi yake
The Fixer bicha maji a.k.a marehemu wa akili akose hata dawa mseto.
Kinachokusumbua wewe ni njaa na nikukumbushe kuwa shilingi elfu mbili mbili mnazopewa Lumumba hazina pension. Uzee wako hautakuwa tofauti na wenzio uliowaacha kijijini ambao hata sasa posho za Lumumba haziwafikii.
Ndugu yangu, Marehemu
The Fixer, lengo hasa la ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO kutamka kuwa itaanzisha mchakato wa katiba mpya, ni kutaka kuondoa huu mfumo wa watu wengi kuwakilishwa na mtu mmoja ambaye si chaguo lao na amepatikana kwa siasa badala ya taaluma.
Ikiwa hilo ndio lengo la CDM, na CCM ikaliiba hilo lengo kwa manufaa ya kulipotosha, CDM hawatakaa kimya. Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Kata walichaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura, hii ikiwa na maana kuwa wananchi wamepewa nguvu ya kuchagua watu wa kuwasilisha mawazo yao, halafu inatokea tena watu 8 (ambao wako influenced na CCM) wanapangua chaguo la wananchi kwa kuwaondoa hawa na kuwaacha wale kwa vigezo visivyo wazi kwa wananchi, basi hapo sioni kama dhana ya katiba mpya inalindwa.
Kwa akili za watu wafu kama wewe, unaweza ukadhani kwamba hili nijambo la kuchekelea kama mlivyozoea kupinga kila kinachosemwa na upinzani. Lakini nakuhakikishia kuwa, hiyo tume ni upotevu wa fedha na muda kama itakavyothibitika kwa
VITAMBULISHO VYA TAIFA. Bado sijafa kifikra kiasi cha kuamini kuwa watu wenye ubongo unaowaza kutumia 1bn kununua makaburi wanaweza kuwa ndio hao hao watu wa kuwa na mawazo yatakayotuletea maendeleo.