Pricing-Kupanga Bei ya Bidhaa na huduma

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Habari za wakati huu;
Leo naona nilete mjadala kuhusu moja ya changamoto ambayo wajasiriamali hukutana nayo katika biashara zao nayo inahusu upangaji wa bei au kwa kimombo "pricing"Katika uchumi wa soko huria tunaamini kwamba Bei hupangwa na soko kwa kuzingatia demand na supply.Ila kuna ukweli wa kiuchumi ambao unasema kwamba kuna kiwango cha chini kabisa cha bei ambacho mzalishaji hatakubali kuuza na kuna kiwango cha juu kabisa amacho mnunuzi hatakubali kunununua.

Unafuu au ughali wa bei huwa unategemea uwezo wa kufanya manunuzi(Purchasing Power) na Gharama za uzalisha (Production Cost).Hata hivyo katika biashara kunakuwa na ushindani hali ambayo inafanya kuwe na umuhimu wa kuwa na competitive advantage au wengine huwa wanapenda kusema siri ya biashara.Ili uwe na siri ya biashara lazima ulielewe soko vizuri ikiwamo wateja wako,washindano wako na zaidi gharama zako za uzalishaji.Ukielewa vizuri katika maeneo hayo matatu na ukawa na taarifa sahihi basi unaweza kufanya Pricing ya uhakika.Je bei nZuri ni ipi?

Be nzuri ni ile ambayo inamwezesha mzalishaji kuendelea kutoa huduma na kuendelea kuwepo sokoni.Yaani aweze kufikia BREAK EVEN.Mfanya Biashara au mtoa huduma anaweza kuendelea kutoa bidhaa au kuzalisha huduma iwapo tu anafikia malengo ya kurejesha gharama zake.

Ili uweze kujua iwapo umerejesha gharama zako lazima uwe mkakati wa kukuwezesha kufahamu unit cost kwa bidhaa au huduma zako.Ndio maana ni muhimu sana kuhakikisha kwamba unajilipa wewe mwenyewe na unatunza kumbukumbu zote kuhusu biashara yako.Unaweza ukawa unafanya biashara unauza milioni 10 kila siku lakini kumbe gharama zako za kuzalisha ni milioni 11 na kama huna takwimu sahihi unaweza usijue.

Je ni mikakati gani ambayo huwa unaitumia katika kuhakikisha kwamba unakuwa na BEI sahihi kwa bidhaa au huduma zako huku ukiendelea kutoa huduma bora?

Tujadili
 
Back
Top Bottom