Ningeomba Mh. Waziri atuweke kinagaubaga ni mgogoro upi wa ardhi ambao umekuwepo zaidi ya miaka 20 iliyopita wakati hiyo ardhi imetengwa kwa ajili ya GCA tangu mwaka 1974? What hapenned in the past 20 years na serikali, given all its powers, kushindwa kuutatua kwa miaka yote hiyo? La sivyo wananchi wana legitimate claims kuhusu hilo eneo!
Mkuu hii issue imeanza tokea kipindi cha ukoloni. Wanahistoria wanasema kuwa wanachofanya serikali ya sasa ni mwendelezo wa kilichokuwa kinafanywa na serikali ya kikoloni, lakini serikali ya sasa inafanya kwa gia ya "investors".
Mwaka 1959, watu wote waliokuwa wanaishi eneo la Serenegeti walifukuzwa na serikali ya kikoloni ya Kiingereza ili kufanya eneo hilo kuwa mbuga ya kitaifa. Baadhi ya watu waliofukuzwa walikuwa ni Wamasai ambao waliishia kwenda kuanza makazi mapya eneo la hifadhi la Ngorongoro na Loliondo.
Baada ya uhuru serikali au watu fulani serikalini wameendelea kuwa na jicho ya ulafi kwa kutenga ardhi kwa ajili ya utalii wa picha na wageni kuwindia wanyama. Kwa sasa ulafi huu uko zaidi Loliondo. Mwaka 1992, Otterlo Business Corporation Ltd (inasemekana hii siyo kampuni bali ni kikundi tuu cha watu kutoka Uarabuni) ilipewa Pori tengefu la Loliondo (Game Controlled Area) kwa ajili ya kuwindia wanyama.
Otterlo Business Corporation Ltd hawana ardhi, bali wamepewa tuu leseni ya kuwinda wanyama kwenye korido ya ardhi inayopakana na hifadhi pori ya taifa. Hata hivyo, kinadharia wanaweza kuwinda mpaka panya kuzunguka ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.
Kila panapokuwa na mgogoro baina Otterlo Business Corporation Ltd na Wamasai, serikali inakuwa upande wa Otterlo Business Corporation Ltd. Utakumbuka nini kilitokea mwaka 2009. Pamoja na kwamba Otterlo Business Corporation Ltd na Wamasai walifikia suluhisho na kurudi kwenye eneo husika, mwaka 2011 serikali ilianza tena chokocho zake kwa kuja na mpango wa kuifanya hiyo korido kuwa pori tengefu, chini ya Sheria ya Hifadhi ya Wanyama No. 5 ya mwaka 2009.
Kipindi cha ukoloni, pori tengefu ilikuwa ni sehemu ya kuwindia wanyama. Hii ni tofauti na sehemu ya wazi (open area) ambayo hairuhusiwi kuwindia wanyama. Kwa vile matumizi ya ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji yalikuwa ni sehemu ya wazi, Game Controlled Area iliangukia kwenye ardhi ya vijiji.
Hili jina la "Game Controlled Area" limeendelea kuwepo hata baada ya uhuru bila kuwa na maana yoyote. Kama walivyofanya wakoloni, serikali ya sasa imeendelea kutumia concept ya "Game Controlled Area" kwa nia ya kuwachanganya watu na kweli imefanikiwa kwa hilo.
Jaribu kujiuliza kwa nini "Game Controlled Area" ziko Tanzana tuu?