Mi mwenyewe sikuamini kama sumaye keshakuwa mufilisi kisiasa namna ile. Anazungumza mafumbomafumbo tuu utadhani mwimbaji wa taarabu. Mara mtandao umeniangusha, mara rushwa, mara sina uadui na Lowasa, mara simuogopi mtu, mara mtu anaweza akanunua mtandao sijui wilaya ngapi, mara ccm sio mama yangu, mara nitafia hapahapa ccm, mara mara sina mpango wa kwenda CDM eti nikitaka nitapitia humuhumu ccm!!!! Sasa kama ukitaka utapitia humohumo, si ndio tayari umeshataka na wamekupiga chini??? unataka utakeje tena??? siamini kama hizi ni kauli za mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu kwenye hii nchi.