Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,370
Tanzania ni vigumu mno au pengine niseme haiwezekani kupiga hatua kwa sababu zifuatazo:
1. Kila serikali inayoingia madarakani inaimba wimbo ule ule wa maendeleo, maendeleo, maendeleo lakini miaka yake kumi inaisha gari limenasa kwenye tope lile lile. Tatizo ni kwamba hakuna anayeona kwamba taifa linapitishwa njia ya mkato kuelekea maendeleo. Maendeleo ni ngazi ya tatu; ya kwanza ni kiwango bora na cha juu cha elimu kwa wananchi na ngazi ya pili baada ya watu kuelimika ni ustaarabu. Bila kupitia hatua hizi mbili za awali wimbo utawahi ule ule. Hakuna serikali yoyote ikiwemo hii ya awamu ya tano ambayo inatambua hili. Kwa kifupi duniani hakuna jamii iliyoendelea pasipo elimu ya hali ya juu na ustaarabu.
2. Kutokuwepo kwa mpango mkuu uliopita endelevu ambao kila serikali itakayoingia madarakani itaanzia pale serikali iliyopita ilikoachia. Wachina wanaandaa mpango mkuu halafu wanaugawa kwa miaka mitano mitano na serikali inayokuwa madarakani inautelekeleza. Mtu anaweza kusema wao wameweza sababu wana serikali ya chama kimoja tu; ni kweli lakini hata sisi pamoja na madai ya kuwepo vyama vingi kimsingi serikali imebaki kuwa ya chama kimoja na itaendelea kuwa hivyo.
Hii ingekuwa fursa kwa watu wa CCM kutengeneza mpango mkuu tangu miaka ya nyuma na kuhakikisha serikali zinazoingia madarakani zinautekeleza. Bahati mbaya kwa uafrika wetu kila anayeingia madarakani a nataka aonyeshe kuwa aliyepita alikuwa henye tu. Hii inasababisha kila baada ya miaka kumi tunaweza moja, ni sawa na mtoto anayecheza kwenye bembea anaenda mbele ubaki huo huo halafu anarudi nyuma ubaki huo huo matokeo yake hasogei.
Kwa mambo haya mawili hatuwezi kupiga hatua kamwe.