President Magufuli Mourns Fidel Castro death

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mauti ya aliyekuwa rais wa Cuba Fidel Castro.

========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016.

Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema;
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.

Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."


Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
 
Mi ninavyoona Gerson Msigwa na Emmanuel Buohera hawatoshi.waachie ngazi graduates wengi kwa sasa!
 
sasa hizo ndio shule zetu, elimu zetu. na bado watu wanataka tudumishe kiswahili badala ya kuamua kuanzia letu toka primary tutumie english tu, watu wangekuwa vizuri, ati uzalendo. putuuu
 
On behalf of myself, siyo kiingereza hicho japo maneno yote ni ya kiingereza.

Hata kusema, 'kwa niaba yangu mwenyewe', siyo kiswahili kizuri, ni upuuzi. Kwa niaba hufanyika na nafsi nyingine bila mhusika mwenyewe kuwepo. Utasemaje kwa niaba yako wakati ni wewe ndiye unayetamka?
 
On behalf of myself, siyo kiingereza hicho japo maneno yote ni ya kiingereza.

Hata kusema, 'kwa niaba yangu mwenyewe', siyo kiswahili kizuri, ni upuuzi. Kwa niaba hufanyika na nafsi nyingine bila mhusika mwenyewe kuwepo. Utasemaje kwa niaba yako wakati ni wewe ndiye unayetamka?

Tumsitiri.
 
Hii inadhihirisha wazi kinachosemwa ni cha kweli kabisa, Mkulu lugha haipandi kabisa.

Haiwezekani kila mara akosee! Hawa wakina msigwa wapo kwa ajili gani?

Hii Akaunt ifike mahali awaachie Wataalamu ndio wawe wanampostia au atumie Lugha ya kiswahili tu inatosha.
 
1480226776099.jpg


Hii lugha ilipanda meli bana.
 
Mbona tunaaibishana jamani watu wa Ikulu huko vipi? Kwanini hamuangalii makosa madogo ya namna hii? Hiyo tweet inatembea dunia nzima halafu juu hapo aliyeandika ni "Dr" (PhD); tena aliyesomea shahada zote kwa kimombo. Yaani ameseomea miaka 16 kwa hiyo lugha (4+2+2+3+2+3=16)
 
Sasa ile research ya Korosho aliandikaje kama ku tweet tu kidhungu kimemshinda?! Au kuna hujuma zinaendelea apo jumba jeupe
 
Back
Top Bottom