Presha Kuka

OleWako

Member
Joined
Sep 7, 2021
Posts
24
Reaction score
67
Kuna supu inayochemka kwenye presha kuka. Ndani yake kuna kuku wa kienyeji, viazi, na ndizi – vyote vimeshaiva tayari. Lakini Mama Ntilie kaenda kando, anakula chapati zake kwa utulivu. Ameketi kwenye kiti chake cha plastiki, cha kijani kibovu. Kiti hicho kimechoka; mguu mmoja ulivunjika jana, akakiwekea chupa ya rum kama tegemeo. Neema ya Mungu kwenye hicho kiti ilishafifia zamani.

Wadudu wanaendesha maisha yao ndani ya jiko lake: mende wanaogelea kwenye mafuta, sisimizi wanabeba kibegi cha sukari polepole, machawa wanacheza ngoma kwenye nywele zake huku panya wakitoroka na mguu wa kuku kuuficha gizani. Lakini Mama Ntilie hana haraka – amejitulia, anafurahia chapati zake laini, alizopika yeye mwenyewe peke yake. Si alikopa tu kwenye kikoba? Basi anaamua aonje jasho lake kwanza.

Presha kuka inaanza kupiga filimbi – si ile ya kawaida, hii inakera hadi inapenya kwenye moyo. Lakini Mama hata hajamaliza chapati yake ya kwanza. Hiyo ni ile nusu iliyobaki ya mteja wake wa mwisho jana, aliyekimbilia daladala bila kulipa.

Anapoudhiwa na kelele, Mama anainuka kwa uzito, anaziba valve kwa kitambaa chake cha kahawia – kimetapakaa mafua ya kale na madoa ya mafuta. Hatimaye, ukimya.

Lakini anachokipuuza ndicho hatari yenyewe: kiegemeo cha kiti chake kimelegea mno, chupa ya rum iliyokuwa msaada tayari imeteleza, na miguu mingine ya kiti imeanza kulegea pia. Je, kweli hiyo miguu mingine itamsaidia? Na mbaya zaidi – hiyo presha kuka sasa imeanza kuguguma. Hiyo si ishara ya mwisho kabla ya mlipuko?

Mama Ntilie, pamoja na kuona haya yote, bado anaendelea kula chapati yake kwa makini. Kama vile hakuna kinachoweza kumtokea. Kama vile maisha hayawezi kumwangukia kwa uzito wake wote.
 
"Mama ntilie" ni mvivu wa kufikiri, pia huenda ana "buzi" linalomuendeshea hiyo biashara ndiyo maana hajitikisi, pamoja na kukuru kakara za hapo, anajifanyia bora liende, hajali kiti kibovu, alichokalia kinaweza muangusha wakati wowote.

#Watakaoelewaniwalioishihavana.
 
Huyo mama ntilie ni mvivu au ni uwezo mdogo wa kufikiria?
 
Kwanini "mama ntilie" ajipigie misosi badala ya kuhudumia "wateja" wake washibe kwanza
 
Pressure kuka ni nin madam? Kwa sisi wasoma headline tu ni tabu sana🤔
 
Watawala wasinyanyase wanaowaongoza

Ki ukweli kabisa, huyu hapana hapana, bora aje mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…