PrecisionAir waanza kujiharibia jina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PrecisionAir waanza kujiharibia jina

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Monstgala, Apr 27, 2012.

 1. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mimi ni mmoja wa abiria tuliokuwa tunaelekea kanda ya ziwa leo hii kwa usafiri wa hawa ndugu zetu waliopata kujitengezea reputation nzuri hapa Tz. Katika hali ya kushangaza tumesimamishwa kwenye queue masaa mawili bila ya huduma huku tukiambia hamna network. Baada ya hapo tumecheck-in alafu tumekaa masaa mengine mawili tukiambiwa ndege imechelewa. Alafu ghafla dada mmoja mhusika katukusanya na kutuambia twende lunch kwa sababu hawana uhakika na ndege hiyo tunayoisubiri.

  Wakati tukiwa tunaburuzwa kwenda "lunch" dada yule kaingiza habari nyingine kuwa abiria wa Musoma safari leo hamna. Wakati abiria tukiambizana kulikoni mwenzetu mmoja katudokeza kwamba haka kamchezo kapya sasa kana wiki.

  Hitimisho: mpaka sasa tupo hapa (masaa matano) tunasubiri hatma yetu na sio siri PrecisionAir wakiendelea hivi reputation waliyoitengeneza kwa muda mrefu itayeyuka na yale ya Air Tanzania yatajirudia.
   
 2. S

  Silent Burner Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamebweteka hawa, baada ya kuona ATCL iko mortuary. Ole wetu tulionunua hisa zao, wakiendelea hivi itakula kwetu.
   
 3. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Duh pole sana rafiki, hako ka mchezo Press on air zamani Precession air wamekaanza siku nyingi zaidi ya mwezi/miwili hivi. Siku moja me nilikuwa miongoni mwa abriria tuliokuwa tunatakiwa kutimka Mza saa9.alasiri lakini tulifika Dar saa 9. usiku. Full kupigwa danadana baadae tukapelekwa kupata midnight dinner LAKAIRO
   
 4. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi wale mlio na taarifa za undani - je hisa za Precision Air zinalipa au watu wameingizwa mkenge kama ilivyokuwa kwa Tanzania Oxygen (TOL)?
   
 5. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu, abiria wamenuna vibaya sana. Wengine wana vitoto vichanga yani ni chaos.
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hivi wale 540 nao huduma zao zikoje?
  Au wanakandege kamoja?
   
 7. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shida ni kwamba hatuna usafiri wa anga mbadala tatizo linaanzia hapo, kwa hiyo they can tell you anything and you will have to agree whether u like it or not.
   
 8. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Maneno ya wahenga MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI yanajionesha sana waswahili tukifanikiwa kufikia namba moja katika mafanikio kwenye nyanja yoyote (tulio wengi; sio wote).

  Hawa Precision wanaona wamekuwa International airline tayari na ndio WAMEWIN=kupuuzia utaratibu na nidhamu iliyowafikisha walipo!

  Sijui lini tutajifunza WAGALATIA sisi!
   
 9. A

  Ahmada umelewa Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwangu walishapoteza mda, washanikosesha International flight huku naona.


  QUOTE=Mgalanjuka;3793851]Mimi ni mmoja wa abiria tuliokuwa tunaelekea kanda ya ziwa leo hii kwa usafiri wa hawa ndugu zetu waliopata kujitengezea reputation nzuri hapa Tz. Katika hali ya kushangaza tumesimamishwa kwenye queue masaa mawili bila ya huduma huku tukiambia hamna network. Baada ya hapo tumecheck-in alafu tumekaa masaa mengine mawili tukiambiwa ndege imechelewa. Alafu ghafla dada mmoja mhusika katukusanya na kutuambia twende lunch kwa sababu hawana uhakika na ndege hiyo tunayoisubiri.

  Wakati tukiwa tunaburuzwa kwenda "lunch" dada yule kaingiza habari nyingine kuwa abiria wa Musoma safari leo hamna. Wakati abiria tukiambizana kulikoni mwenzetu mmoja katudokeza kwamba haka kamchezo kapya sasa kana wiki.

  Hitimisho: mpaka sasa tupo hapa (masaa matano) tunasubiri hatma yetu na sio siri PrecisionAir wakiendelea hivi reputation waliyoitengeneza kwa muda mrefu itayeyuka na yale ya Air Tanzania yatajirudia.[/QUOTE]
   
 10. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni kitu cha kawaida hicho katika usafiri wa anga na ndio maana wana rekodi nzuri ya usalama kazini au ndege yao kuleta mushkeli.Tatizo wabongo mnataka kila kitu asilimia 100% perfect on time wakti siyo kweli.Nchi yetu ni kubwa na shirika hivi sasa linahudumia na abiria waliokuwa ATCL.Tunaosafir na Pression kila mara ni kitu cha bahati mbaya tu hicho.Kwa kuwa wewe unafiri mara moja baada ya miezi sita au mwaka umeona nongwa wakti sisi kila wiki au mwezi mambo yao uwa tambarare tu.
   
 11. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Ngoja ni wa google wanandege ngapi, ila nafikiri bei zao ziko juu kidogo alafu unalipa in USD.
   
 12. S

  Silent Burner Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huna haja ya kutumia ID ya kificho, weka kabisa kwamba wewe ni AFISA UHUSIANO WA PRECISION AIR.
  Haya, endelea kulinda uoza wenu.
   
 13. F

  Fofader JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Ni kama daladala! Kama imejaa inaondoka kama abiria hawajajaa mnasubiri mpaka wapiga debe wajaze watu.
  Hii ndio TZ.
   
 14. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kanga, hakuna sehemu niliyoandika kwamba mimi nasafiri mara moja tu na bahati mbaya sana hunijui hivyo you are totally wrong unapojaribu kunishambulia mimi badala ya hoja iliyopo. Ungenifamu vizuri hizo majigambo za kitoto ungewasubiri wengineo. By the way, kwa kuwa sisi ndio waathirika wa hizi "bahati mbaya" tuna haki zote za kusema ukweli. Kwa taarifa yako tumedokezwa kwamba "all this was already known but they were buying time and find a smooth way to tell us" so bahati mbaya doesn't really fit here.
   
 15. G

  GWATABHIKURUME Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hawa watu kama wameanza kuharibu waambiwe tu, hili shirika lilkuwa la kutegemewa sana hapa Tz lakini kama mipango imeanza kuwa hivi inaogopesha sasa kama huyu ndugu yangu aliyekoseshwa International Flight si ni kipigo balaa! Ila mambo kama haya hata kwa wenzetu yanatokea japo wao wana njia nyingi za kutafuta suluhu chapchap nakumbuka niliwahi ku miss International flight Zurich Switzerland kwa sababu ya delay ya one hour Amsterdam to Zurich lakini nilikuwa handled vizuri sana.
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nikikujibu nitaambulia ban. Siku hizi huwa naona ni bora nipande green star kuliko precision, nimekuwa muhanga wa precision mara 7 ndani ya miaka 2.5 ukiachilia kupoteza masaa 2 au 3 ndio usiseme. Imekuwa ni utamaduni sasa
   
Loading...