Sipo unakumbuka mambo ya enzi zileeee, wakati hata hakuna kitu kinachoitwa tuisheni, pre-unit, baby -class, middle-class na madude mngine meeeengi!
Kwa mtazamo wa haraka haraka utasema kwamba siku hizi hali ya uelewa wa watoto imeshuka, lakini kutokana na mabadiliko mengi ya kijamii na kiteknolojia, na ongezeko kubwa la watu, kumezaliwa mashindano makali sana ya fursa mbalimbali za maisha, likiwemo ndani suala la hizo pre-something.
Akili za watoto wa saa zinakuwa occupied na mambo mengi ya starehe na uhuni, mambo ya meseji za mapenzi, tv, tarakilishi etc.hivyo ni lazima mwisho wa siku mtoto huyu anatindikiwa upande fulani.