Pray for Russia, tuache ushabiki

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,145
Reaction score
3,765
Tuwekeni ushabiki pembeni.
Yalioko kwenye uwanja wa mapambano yanatisha.

Askari wa Russia wanaokamatwa katika uwanja wa mapambano wanafanyiwa unyama wa hali ya juu, tunaiomba Ukraine irudishe moyo nyuma kwani hao nao ni binadamu wenzao pia.

Picha na video nimeshindwa hata kuziangalia mara mbili neno ubinadamu katika jeshi la ukraine wameliondoa kabisa, Ukraine haina muda tena na mateka ndo mana huskii idadi ya wanaotekwa
yaani hadi unaona watu wazima wanaacha silaha wanavua gwanda wanakimbia jua hali ni mbaya.

Askari wa Russia wanachofanyiwa sote tuungane tuache upro usio na maana ni unyama wa hali ya juu tulaani kwa sauti moja.

Tunaomba Marekani, NATO na Dunia kwa ujumla kuingilia kati tena kwa upya. Ukraine wanawafanyia unyama wa Kutisha askar wa Russia. kwa kuangalia picha na video ambazo baadhi zipo humuhumu binafsi ninaona hata aibu kujiita binadamu mbele ya Viumbe wengine.

Tuombee majeshi ya Russia watoroke kwa amani, video na picha nmeshindwa kuzipost sababu ni mbaya kwakwel nafsi inanisuta hata kuwaonesha.

waamdish wa habari wamezuiwa kwa muda kuingia maeneo yenye counteroffensive ya Ukraine. maana wsione jinsi ukraine inawafanyia askar wa russia ambao wangeweza kuwafanya mateka lakin badala yake ni michinjo tu.

maeneo mengine imebid askar wa Russia kujichanganya na Raia kwa kuvua geanda.

Hata kama ni vita hiii ni too much.
UKRAINE. rudisha moyo nyuma baba.
kusamehe ni ibada.

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alimtaka Rais wa Urusi Vladimir Putin kuingia tena kwenye meza ya mazungumzo na Ukraine haraka iwezekanavyo wakati wa mazungumzo ya simu ya dakika 90 siku ya Jumanne.

hivi tunavyooongea UKRAINE wanabisha hodi DONBAS.
 
We jamaa sijui unawazaje wewe. Huo ubinadamu unauona kwa wa Rashia tu kutendewa sio. Labda nikuulize swali dogo tu, hao askari wanaokamatwa wanakamatiwa wapi Rasha au Yukreni?

Wameenda kufanya nini Yukreni au kutembea tu vakasheni? Yaani mtu anakuja kwako na masilaha kukuua tena kwako alafu ukimkamata unaombwa uwe na huruma ilhali wewe usingejiwahi yeye angekuua, theory ya wapi hii mkuu?

Dawa ni kuwaomba Yukreni wawe na huruma au kuwaomba Rasha watoke nchi ya wenyewe.
 
We jamaa sijui unawazaje wewe. Huo ubinadamu unauona kwa wa Rashia tu kutendewa sio. Labda nikuulize swali dogo tu, hao askari wanaokamatwa wanakamatiwa wapi Rasha au Yukreni?...

Hapana kwa kweli warudi tu kwenye meza ya Mazungumzo wamsetiri Putin.
hii ni Aibu. hata kuku ananamna yake ya kuchinjwa.
 
πŸ˜€πŸ˜€,kwahiyo tutegeme Russia kufurumushwa Donbas na Crimea muda si mrefu?

Uzuri Russia haweki hadhari picha za wa Ukraine wanaokufa,angefanya hivyo watu mngekimbia humu!
Fikiri kama kukomboa sqkm 6000,basi ndio Ukraine anachukua picha za kutamba nazo,vp Russia aliyechukua Sqkm zaidi ya laki,wamekufa wa Ukraine wangapi?

Russia mpaka alikuwa anachimba makaburi ya halaiki anapakia waukraine,ila hakutaka pich kuweka hadharani!

Tatizo Ukraine, anataka kuishinda vita ya kwenye media tofauti na uhalisia ndio maana hata akiua askari watano basi picha kwanza na inatumwq mitandaoni!
 
πŸ˜€πŸ˜€,kwahiyo tutegeme Russia kufurumushwa Donbas na Crimea muda si mrefu?
Uzuri Russia haweki hadhari picha za wa Ukraine wanaokufa,angefanya hivyo watu mngekimbia humu...
Ngoja tuuone mwishowe.
 
Tuwekeni ushabiki pembeni.
Yalioko kwenye uwanja wa mapambano yanatisha.

Askari wa Russia wanaokamatwa katika uwanja wa mapambano wanafanyiwa unyama wa hali ya juu, tunaiomba Ukraine irudishe moyo nyuma kwani hao nao ni binadamu wenzao pia...
Mkuu upo hapo Ukraine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…